Wednesday , 24 April 2024
Home Kitengo Maisha Afya Ufahamu ulemavu wa miguu kifundo na madhara yake
AfyaMakala & Uchambuzi

Ufahamu ulemavu wa miguu kifundo na madhara yake

Spread the love

SIKU ya miguu kifundo au nyayo za kupinda ulimwenguni huadhimishwa kila mwaka tarehe 3 Juni. Tarehe hii ilitokana na maadhimisho ya siku ya kuzaliwa ya Dk. Ignacio Ponseti, (1914-2009) Daktari aliyegundua njia ya kutibu ulemavu huo ijulikananayo kwa lugha ya kingereza kama “Ponseti method”.

Lengo la Siku hii ya Mguu kifundo ni kukuza uelewa juu ya ulemavu huu  na kuhamasisha utumiaji wa matibabu yake kwa kutumia njia ya Ponseti.

Miguu kifundo au nyayo zilizopinda ni nini?

Mguu kifundo au nyayo za kupinda ni aina ya ulemavu wa mguu au nyayo  ambapo mguu mmoja au yote huelekea ndani na kwa kutazama chini. Hali hiyo inaathiri mifupa, misuli, ngozi na mishipa ya damu ya mguu/unyayo. Hili tatizo ni la kuzaliwa nalo, na huathiri watoto wa kiume zaidi kuliko wale wa kike .Sababu ya kuwaathiri watoto wa kiume kuliko wale wa kike bado haijajulikana na tafiti zinaendelea.

Ukubwa wa tatizo, Ulimwenguni

Tafiti zinaonyesha kuwa mguu kifundo au nyao za kupinda hutokea kwa mtoto 1 kati ya 750 aliyezaliwa hai kila mwaka. Duniani kote takribani  watoto 813,000 huzaliwa na mguu kifundo kila mwaka na 80% ya hizi ni hutokea  nchi zinazoendelea hususani  Kusini mwa Jangwa la Sahara hii ni sawa na (22%).

Tanzania

Kwa mujibu wa tafiti watoto 2200 hadi 3000 wanazaliwa na mguu kifundo/nyayo za kupinda  kila mwaka hapa nchini. Kwa mujibu wa Dokta Zainab Illonga  daktari wa mifupa kutoka hospitali ya  CCBRT Dar es Salam, hospitali hiyo huwaona watoto na watu wazima  wapya wenye matatizo hayo takribani 400  kwa mwaka.

Ni nini husababisha ulemavu huu?

Hakuna sababu kubwa ambayo husababisha mguu kifundo au nyayo za kupinda ingawa kuna sababu kadhaa ambazo huweza kuchangia mtoto azaliwe na mguu kifundo/nyayo za kupinda. Miongoni mwazo ni, uhusiano wa kifamilia kama kuna mtu ndani ya ukoo/familia aliwahi zaliwa na aina hiyo ya ulemavu inaweza jitokeza kwa mtoto anayezakiwa baadae katika familia hiyo.

Sabu nyingine ni pamoja na ukaaji wa mtoto kwenye mfuko wa uzazi, shida ya mfumo wa fahamu kama ugonjwa wa kupooza kwa ubongo na mgongo wazi Kiasi kidogo cha amniotic kinachomzunguka mtoto kwenye mfuko wa uzazi (oligohydramnios) wakati wa uja uzito yaweza kuwa sababu ya mtoto kuzaliwa na tatizo hilo.

Je! Kuna dalili gani za mguu kifundo?

Dalili za mguu kifundo ni Mguu kuonekana mfupi na mpana, kisigino huelekea chini wakati nusu ya mbele ya mguu (mguu wa mbele) hugeuka ndani.

Msuli kamba wa kisigino (Achilles tendon) unakaza na mfupi.

Kisigino kinaweza kuonekana chembamba. Misuli ya mguu ni midogo ikilinganishwa na mguu wa kawaida.

Je! Mguu kifundo hutambuliwaje?

Mtoa huduma ya afya kwa mama na mtoto anaweza kutambua hitilafu ya nyayo za mtoto mara baada ya kuzaliwa na hivyo kushauri mahali pa kumpeleka kwa matibabu ya mapema.

Pamoja na hilo mlezi au mzazi anaweza tambua dalili hizo za mtoto mwenye nyayo za kupinda wakati wa malezi na makuzi ya mtoto. Endapo atafikishwa kwenye huduma wakati muda umekwisha pita sana kunaweza kuwa na ulazima wa kupiga mionzi (X ray) ili kubaini shida zaidi.

Je! Mguu kifundo unatibiwaje?

Matibabu hutegemea dalili za mtoto , umri, na afya yake kwa ujumla. Pia itategemea jinsi hali ilivyo. Lengo la matibabu ni kunyoosha mguu ili uweze kukua na kuimarika na kuwa kawaida. Bila matibabu, mtoto atakuwa na shida kwenye kutembea.

Matibabu ni pamoja na:

Njia ya Ponseti (bila upasuaji mkubwa) (Dr Ignacio Ponseti, mvumbuzi wa mbinu ya Ponseti kwa ajili ya matibabu ya mguu kifundo)

Hii kawaida hujaribiwa kwanza bila kujali ukubwa wa tatizo. Matibabu haya yanatumia utaalamu wa kunyoosha misuli kwa utaratibu maalumu kisha kufunga hogo kila baada ya wiki moja ili kurekebisha mguu hatua kwa hatua.

Mara nyingi huchukua mwezi mmoja hadi miwili kisha mtoto anaweza akahitaji upasuaji mdogo wa kulegeza msuli kamba wa kisigino na kisha kufungwa hogo la mwisho. Baada ya hapo kwa sababu mguu kifundo huweza jirudia mtoto atalazimika kuvaa viatu maalumu kwa miaka kadhaa ili kuzuia mguu usirudi tena. Mara ya kwanza, viatu hivi huvaliwa kwa masaa 23 kwa siku hadi miezi 3. Halafu huvaliwa usiku tu hadi miaka 5.

Mtoto mwenye tatizo hilo anaweza kuhitaji upasuaji mkubwa ikiwa matibabu mengine hayarekebishi mguu. Upasuaji maalum unategemea aina na kiwango cha hitilafu cha mguu na umri wa mtoto.

Watoto wengi wachanga walio na mguu kifundo hawahitaji upasuaji. Watoto ambao huhitaji upasuaji huenda wakahitaji  upasuaji zaidi ya  mara moja kwa sababu hitilafu ya mguu yaweza kurudi kadri anavyokua.

Ni nini kinatokea ikiwa mguu kifundo/nyayo za kupinda imeachwa bila kutibiwa?

Ikiwa mguu kifundo haukutibiwa mtoto hataweza kutembea kawaida. Wakati mwingine inawezekana kutembea na mguu kifundo, lakini ni ngumu sana.

Watoto ambao wana mguu kifundo hutembea kwa upande wa juu ya miguu yao. Hii inaweza kusababisha kovu kubwa na maumivu sugu.

Mtoto anapokua na kujitegemea kimaisha kuwa na mguu kivundo itamaanisha kuwa na changamoto katika shughulli zake za kila siku na hata uwezo wa kuzalisha kipato.

Je! Matibabu ya  mguu kifundo  hutolewa wapi?

CCBRT na hospitali washirika hutoa matibabu hayo, kwa CCBRT matibabu  kwa watoto chini ya miaka mitano hutolewa bila malipo. Hospitali hii ina uzoefu wa kufanya matibabu ya aina hii kwa takribani miaka 19.

Je! Unaweza kushauri nini jamii kwa ujumla juu ya mguu kifundo?

Mguu kifundo unatibika na sio kurogwa wala laana. Wazazi wawapeleke watoto hospitalini kupata huduma mapema iwezekanavyo. Wakunga wawachunguze watoto wachanga na wale watakaobainika na mguu kifundo wawaelekeze kwenda CCBRT au hospitali inayotoa huduma sahihi ya mguu kifundo.

Tunashauli pia wanasayansi na wanataaluma kujikita pia kufanya utafiti zaidi kuhusu mguu kifundoTanzania. Pia tunatoa wito kwa wafadhili wajitokeze zaidi ili kuweza kuhakikisha hizi huduma zinaendelea kutolewa bure.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaMakala & Uchambuzi

Kanda ya Ziwa yaonyesha NMB inavyosaidia afya ya mama na mtoto

Spread the loveMafanikio inayozidi kupata Tanzania katika kupunguza vifo vya mama na...

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

‘Mwanapekee’ wa Rais Samia: Atabadili nini Arusha?

Spread the loveMAPEMA wiki hii, baadhi ya viongozi walioapishwa na Rais Samia...

Habari MchanganyikoMakala & Uchambuzi

Kipunguni waihoji serikali, ziko wapi fedha za fidia?

Spread the loveWATU wanaodai kwamba serikali ya Chama Cha Mapinduzi ni sikivu,...

Habari za SiasaMakala & UchambuziTangulizi

Askofu Bagonza: Tusichonganishwe; tusichokozane na tusikufuru

Spread the loveJOTO la chaguzi linapanda kila siku hapa nchini. Upo umuhimu...

error: Content is protected !!