January 21, 2021

Uhuru hauna Mipaka

UEFA yapanga makundi Euro 2021

Timu ya Ureno ikishangilia ubingwa wa Kombe la Ulaya mwaka 2016

Spread the love

SHIRIKISHO la soka Barani Ulaya UEFA imeendesha droo kwa timu 24 ili kupata makundi kwa ajili ya michuano ya kombe la EURO ambayo inatarajiwa kuchezwa mapema mwakani 2021. Anaripoti Kelvin Mwaipungu, Dar es Salaam … (endelea).

Michuano hiyo ambayo hapo awali ipangwa kuchezwa Juni 2020 na baadae iliahilishwa kutokana na mlipuko wa ugonjwa wa Covid-19 mpaka 2021.

Makundi hayo ambayo yapo sita na kila kundi litakuwa na timu nne ambapo kila kundi litatoa timu mbili ambazo zitaingia kwenye hatua ya mtoani.

Kwenye kundi A kutakuwa na timu za Uturuki, Itaria, Wales na Uswizi huku kundi B, limesheheni timu za Denmark, Finland, Ubelgiji na Urusi, kwa upande wa Kundi C, kuna nchi za Uholanzi, Ukraine, Austria na Macedonia ya Kaskazini.

Kundi D, kuna timu za Uingereza, Croatia, Scotland na Jamhuri ya Czech, huku kundi E, wapo Hispania, Sweden, Poland na Slovakia na kundi F ambalo la mwisho kuna timu za Ureno, Ufaransa, Ujerumani na Hungary.

error: Content is protected !!