January 24, 2021

Uhuru hauna Mipaka

UEFA yaitoa Man City kifungoni

Spread the love

SHIRIKISHO la mpira wa miguu barani ulaya (UEFA) imeifungulia klabu ya Manchester city kutoka kwenye kifungo cha kutoshiriki michuano ya klabu bingwa barani humo kwa ngazi ya klabu kwa kipindi cha miaka miwili. Anaripoti Kelvin Mwaipungu… endelea

Timu hiyo ilifungiwa 14 februari, 2020 kwa kosa la kuvunja sheria za EUFA za leseni ya klabu na matumizi ya pesa na kupigwa faini Tsh. 74.9 Bilioni.

UEFA ilifungua uchunguzi huo baada ya kuwepo madai kuwa klabu hiyo imevunja vifungu kadhaa ya Sheria ya fedha iitwayo ‘Financial Fair Play – FFP’, lakini Klabu hiyo ilikana madai hayo na kusema haijavunja sheria yoyote

Sheria hiyo ilitengenezwa kuhakikisha kiasi cha fedha kinachotolewa na klabu katika kumnunua mchezaji na katika kumlipa vinakaribia kuwa sawa na kiasi mchezaji anachopata katika matangazo na fedha za tuzo

Mara baada ya kutoka adhabu hiyo, uongozi wa klabu hiyo uliamua kukata rufaa kwa mamlaka husika ndani ya shirikisho hilo na baada ya miezi mitano wakafanikiwa kushinda rufaa hiyo.

Timu ambayo kwa sasa inashika nafasi ya pili kwenye Ligi Kuu nchini England na hivyo itafaninikiwa kushiriki michuano ya klabu bingwa barani Ulaya.

error: Content is protected !!