Wednesday , 24 April 2024
Home Kitengo Habari Afrika Uchaguzi Uganda: Museveni ateua mwanajeshi kusimamia usalama
Afrika

Uchaguzi Uganda: Museveni ateua mwanajeshi kusimamia usalama

Yoweri Museveni
Spread the love

YOWERI Kaguta Museveni, Rais wa Uganda, ameamua kumteua Brigedia Kayanja Muhanga, kusimamia masuala ya usalama wakati huu kuelekea uchaguzi mkuu nchini humo unaotarajiwa kufanyika tarehe 14 Januari 2021. Inaripoti mitandao ya kimataifa…(endelea).

Uteuzi ho unampa nafasi Brig. Muhanga kuratibu vikosi vyote vya usalama nchini humo ambavyo vitasubiri sauti yake katika utekelezaji wa jambo lolote.

Luteni Deo Akiiki ambaye ni Naibu Msemaji wa Jeshi la Uganda amesema, Brig. Muhanga atakuwa mratibu wa operesheni za vitengo vyote ikiwa ni pamoja na vikosi vya polisi, jeshi na idara ya ujasusi na usalama.

‘Ni kweli kwamba, Brigedia Kayanja Muhanga amepewa nafasi ya kuratibu vikundi vyote vya usalama kwa madhumuni ya kuunganisha shughuli ya usalama wa pamoja hususan katika Mji wa Kampala na nchi yote,’ amenukuliwa Luten Akiiki.

Kuelekea uchaguzi mkuu nchini humo, Tarehe 17 Desemba 2020, Rais Museveni alimteuwa mwanaye Luteni Jenerali Muhoozi Kainerugaba kuwa mkuu wa kikosi cha ulinzi wa Rais (SFC).

Jenerali Muhoozi, ni mtoto wa kwanza wa rais huyo ambaye amekuwa madarakani kwa miongo minne sasa.

Kabla ya uteuzi huo, Jenerali Muhoozi, alikuwa mshauri wa baba yake – Rais Museveni – katika masuala ya ulinzi.

Mabadiliko hayo yamefanyika katika kipindi ambacho taifa hilo la Afrika Mashariki, linatuhumiwa na mataifa ya Magharibi na Ulaya, kwa ukiukwaji wa haki za binadamu.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

AfrikaHabari

Majenerali 35 kustaafu kutoka jeshi la Uganda

Spread the loveTAKRIBANI majenerali 35 wanatarajia kustaafu kutoka jeshi la Uganda (UPDF)...

AfrikaKimataifa

Gavana wa Benki Uganda afariki dunia

Spread the loveGAVANA wa Benki ya Uganda, Emmanuel Tumusiime-Mutebile amefariki dunia akiwa...

AfrikaKimataifa

Ruto, Mudavadi waungana uchaguzi mkuu Kenya

Spread the loveMakamu wa Rais wa Kenya, William Ruto amethibitisha rasmi kuwa...

error: Content is protected !!