Saturday , 20 April 2024
Home Kitengo Habari Kimataifa Uchaguzi mkuu wa Marekani: Joe Biden, aidhinishwa rasmi kuwa Rais
Kimataifa

Uchaguzi mkuu wa Marekani: Joe Biden, aidhinishwa rasmi kuwa Rais

Joe Biden
Spread the love

Bunge limeBUNGE la Marekani, limemuidhinisha rasmi, Joe Biden, kuwa rais mpya wa taifa hilo kubwa kiuchumi ulimwenguni na Kamala Hariss, kuwa makamu wake wa Rais. Anaripoti Mwandishi Wetu kwa msaada wa mashirika ya kimataifa…(endelea).

Congress limetangaza uamuzi huo baada ya upigaji kura uliofanywa leo tarehe 7 Januari 2021, ambapo kura 282 ziliridhia huku wabunge (kura) 138 wakipinga matokeo ya jimbo la Pennsylvania na Arizona.

Akitangaza matokeo hayo, Seneta wa Minnesota, Amy Klobuchar alisema, “ripoti tunayoieleza hapa ni kwamba, Joe Biden atakuwa ndiye Rais wa Marekani na Kamala Harris, atakuwa makamu wake.”

Ameongeza: “…hii ni kutokana na kura zilizopigwa na wajumbe wa Bunge la Congress na matokeo yaliyopatikana.”

Hatua ya Bunge kumuidhinisha Biden, imekuja siku moja, baada ya wafuasi wa Rais Trump kuvamia Bunge, kwa lengo la kuzuia rais huyo mteule kuidhinishwa na Trump kuendelea kubaki madarakani.

Kitendo hicho, kimesababisha kuibuka kwa ghasia na mauwaji. Katika ghasia hizo, watu wanne, akiwamo mwanammke mmoja, aliyepigwa risasi wakati wa vurugu hizo, wameripotiwa kufariki dunia.

Mtu mwingine amepigwa risasi wakati wa vurugu zilizotokea ndani ya Bunge la Marekani, kulingana na shirika la habari la Associated Press.

Aidha, ghasia hizo zilisababisha shughuli za Bunge hilo kughairishwa baada ya uvamizi huo uliochagizwa na taarifa za Trump, kwamba aliibiwa kura katika uchaguzi uliyopita na hivyo, hakunaliani na matokeo yaliyotangazwa.

Biden alilaumu ushawishi unaofanywa na Trump kutaka kuwaaminisha baadhi ya raia kuwa aliibiwa kura kwenye uchaguzi mkuu wa mwishoni mwa mwaka jana.

Polisi jijini humo wameeleza, waandamaji hao walikuwa tayari kutumia nguvu ili kuingia katika jengo la Bunge.

Waandamanaji hao walikuwa wakiimba “tunamtaka Trump” huku wengine wakisema, “hatukubali aondoke.”

Hata hivyo, taarifa zinaeleza baada ya wafuasi hao kuondoka kwenye jengo la Bunge, shughuli ziliendelea usiku kucha tofauti na muda ulivyopangwa.

Mwandamanaji mmoja aliruka kutoka juu na kuingia moja kwa moja ndani ya ukumbi wa Bunge.

Maafisa wa polisi walikabiliana na wafuasi wao huku baadhi yao wakijeruhiwa.

Wafuasi wa Donald Trump wenye hasira wamevuka mipaka ya usalama iliyowekwa na kusimama kandokando ya Bunge huko Washington, wakati wabunge wanakutana kumuidhinisha Rais mteule Joe Biden kama mshindi wa uchaguzi uliofanyika Novemba mwaka jana.

Katika matukio ya kutatanisha, waandamanaji walizunguka jengo la bunge huku wabunge nao wakisindikizwa kutoka bungeni humo na polisi.

Bwana Biden alisema huo ni “uasi”, huku Bwana Trump kwa upande wake akatoa ujumbe kwa njia ya video akiwataka wafuasi wake kutoka bungeni na kurejea nyumbani.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

KimataifaTangulizi

Mkuu wa majeshi Kenya afariki, Ruto atangaza maombolezo

Spread the loveRais wa Kenya, William Ruto ametangaza maombezo ya siku tatu...

Kimataifa

Majaji kuamua hatima ya Zuma leo

Spread the loveMajaji nchini Afrika Kusini leo Jumanne wataamua ikiwa rais wa...

Habari za SiasaKimataifa

Spika Afrika Kusini ajiuzulu kwa tuhuma za rushwa

Spread the loveSpika wa Bunge la Afrika Kusini, Nosiviwe Mapisa-Nqakula ametangaza kujiuzulu...

Habari MchanganyikoKimataifa

Tetemeko la ardhi laua 7, lajeruhi 800 Taiwan

Spread the loveWatu wapatao saba wamefariki dunia na wengine zaidi ya 800...

error: Content is protected !!