Tuesday , 23 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Uchaguzi Mkuu: ACT-Wazalendo, Chadema nguvu moja
Habari za SiasaTangulizi

Uchaguzi Mkuu: ACT-Wazalendo, Chadema nguvu moja

Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa Chadema
Spread the love

VIONGOZI wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) na Chama cha ACT-Wazalendo, wapo kwenye meza ya mazungumzo ya kuunda nguvu moja ili kuing’oa CCM madarakani. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).

Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa Chadema Taifa, amewaeleza wajumbe wa Mkutano wa Baraza Kuu la chama hicho leo tarehe 3 Agosti 2020 katika Ukumbi wa Mliman City, Dar es Salaam kwamba Chadema na ACT-Wazalendo kwa sasa vinapanga mashambulizi ya kisiasa dhidi ya CCM.

“Hatutaingia kwenye ushirikiano kama fasheni, tutaingia kwenye ushirikiano kama kuna watu wako makini ambao hawatatuuza njiani, tunakubaliana jamani?

“Tunaendelea na mazungumzo lakini niseme bayana, katika mazungumzo tunayoendelea nayo, tunaendelea na mazungumzo na chama cha ACT-Wazalendo,” amesema Mbowe na kuongeza:

“Tutavuna nini inategemea kila mmoja atakuja na mawazo gani. Tunazungumza vilevile kuachiana nafasi ya urais Zanzibar, hayo yote ni mazungumzo yanaendelea.”

Zitto Kabwe, Kiongozi wa ACT-Wazalendo

Mbowe amesema, katika mazungumzo hayo, Chadema iko tayari kuachia nafasi za kugombea.

“Huko nyuma tuliingia kwenye mazungumzo ya ushirikiano wa vyama vingine, miongoni mwa sababu ni unyonge wa chama chetu katika baadhi ya maeneo,” amesema.

Mbowe amesema, Chadema kinaweza kuwa chama kikubwa lakini kinapaswa kuheshimu mawazo ya chama kingine ambacho kinataka kushirikiana nacho.

“Tumheshimu kila mwenzentu kwa ukubwa wake, ukubwa wetu utujengee unyenyekevu usitujengee kiburi, tunapoona kuna sababau ya kushirikiana, tutashirikiana na tukiona hakuna maslahi mapana ya chama na taifa letu, tutafikiria tofauti,” amesema Mbowe.

Tundu Lissu (kushoto) akijadiliana jambo na Lazaro Nyalandu

Ushirikiano ulioundwa na vyama vya upinzani kwenye Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2020, uliacha makovu baada ya kuingia mgogoro miongoni mwa vyama hivyo.

Vyama hivyo viliunda umoja uliotokana wakati wa Bunge la Katiba na kuitwa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa).

Hata hivyo, umoja huo uliingia nyufa baada ya Edward Lowassa, aliyekuwa kada wa CCM kuhamia Chadema na kuteuliwa kugombea urais na kisha kuungwa mkono na vyama vilivyokuwa chini ya umoja huo.

CUF ambacho mwaka 2015 kilikuwa sehemu ya Ukawa, kiliingia katika mgogoro kwa viongozi wake wakuu (Maalim Seif Sharif Hamad, aliyekuwa Katibu Mkuu wa chama hicho na Prof. Ibrahim Lipumba, Mwenyekiti wa CUF Taifa).

Mgogoro huo, ulisababisha Prof. Lipumba kujiuzulu uenyekiti muda mfupi kabla ya uchaguzi, kisha alirejea baada ya uchaguzi na kuibua mgogoro ndani ya chama hicho, jambo lililosababisha ushiriki wa chama hicho na vyama vingine kuwa mgumu.

Dk. Willibrod Slaa, aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chadema, naye alijiuzulu kupinga ujio wa Lowassa kutoka CCM na kuteuliwa kugombea urais kupitia chama hicho.

Kwa sasa Chama cha NCCR-Mageuzi hakina uhusiano mzuri na Chadema kutokana na tuhuma kwamba, kinatumika kuua chama hicho.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mwekezaji amwaga bil. 39 kujenga viwanda 3 vya uchenjuaji

Spread the loveKampuni ya Mineral Access System Limited (MAST) inayoiwakilishwa kampuni ya...

Habari za SiasaTangulizi

Mpwa wa Magufuli mbaroni kwa kusambaza picha za utupu

Spread the loveJESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limewakamata...

Habari za Siasa

Serikali kuanzisha mradi wa Gridi ya maji ya Taifa

Spread the loveWaziri wa Maji, Jumaa Aweso amesema katika mwaka wa fedha...

Habari za Siasa

Rais Samia aridhishwa utendaji mabalozi, awapa neno

Spread the loveRais wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan amewapongeza mabalozi  wanaowakilisha ...

error: Content is protected !!