Saturday , 20 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Uchaguzi Mkuu 2020: DC Dodoma awapa ujumbe wanawake
Habari Mchanganyiko

Uchaguzi Mkuu 2020: DC Dodoma awapa ujumbe wanawake

Spread the love

WANAWAKE wametakiwa kusaidiana katika mchakato unaoendelea wa Uchaguzi Mkuu wa Tanzania utakaofanyika Jumatano tarehe 23 Septemba 2020. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea).

Pia, viongozi wa dini nchini humo, wameombwa kuwahimisha waumini wanaowaongoza kujitokeza kushiriki kuchagua viongozi katika uchaguzi huo.

Wito huo ulitolewa jana Jumanne tarehe 22 Septemba 2020 na Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mjini (DC), Josephat Maganga alipokuwa akifungua kongamano la viongozi wa dini na siasa kuhusu kuhamasisha amani na haki.

Kongamano hilo lilikuwa likiangazia nafasi ya mwanamke kuelekea Uchaguzi Mkuu wa 2020 katika mustakabali wa haki, heshima, amani na utulivu na kuchagua viongozi bora katika mradi wa ‘wanawakesasa.’

“Uamuzi huu wa kuendesha kongamano hili unaakisi lengo kubwa la serikali ambalo lengo ni kudumisha amanina umoja kwa nchi yetu.”

Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mjini (DC), Josephat Maganga

“Kushiriki katika uchaguzi  ni fursa kwa wananchi kuchagua viongozi bora hivyo basi taasisi za kidini zinapaswa kuhimiza amani na upande wa vyama vya siasa vizingatie usawa na haki kwa wanawake kushiriki  kikamilifu,” alisema Maganga.

Mkuu huyo wa wilaya alisema “kumekua na mwamko mkubwa sana wa wanawake wenye sifa stahiki, kushiriki katika kugombea nafasi mbali mbali za uongozi. Hii inadhihirisha elimu ya usawa katika kushiriki masuala mbalimbali ya maendeleo.”

Alisema wanawake waliopata nafasi, wameweza kuzitendea haki nafasi zao jambo linalochochea ujasiri wa akina mama kuongezeka.

“Kuna changamoto mbalimbali zinazowakabili wanawake kuelekea kushiriki katika mchakato wa uchaguzi. Hivyo ni wakati sasa wanawake kuinuana kwa kuungana kwa pamoja kushirikiana katika kugombea nafasi mbalimbali,” alisema Maganga.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania (Tamwa), Rose Reuben alisema, wanaliombea Taifa likatawaliwe na upendo, amani na mshikamano kabla na baada ya uchaguzi mkuu.

“Vyama vya siasa vitambue vina wajibu wa kulinda, kutetea na kudumisha haki na usawa wa wanawake ndani ya vyama vyao katika jamii kwa ujumla, kwa kuwa wanawake ndiyo kundi kubwa la wapiga kura Tanzania,” alisema Rose.

Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania (Tamwa), Rose Reuben

Alisema yapo mapengo mengine yanayorudisha nyuma ushiriki wa wanawake katika siasa na ngazi za maamuzi kwa kumthamini mwanaume zaidi hususan kwenye majimbo ambayo chama kina matarajio makubwa ya ushindi.

“Ipo pia mitazamo hasi katika jamii kuwa mwanamke anapoingia kwenye siasa, basi amejishushia heshima na hadhi yake kwani hakuumbwa kuwa kiongozi, hayo yote yanachangia kupunguza idadi ya wanawake viongozi,” alisema.

Mkurugenzi huyo alisema “rushwa ya ngono, mila na desturi kandamizi, sera zisizo na usawa ndani ya vyama vya siasa, mitazamo hasi katika jamii ni matatizo yanayowakabili wanawake katika ushiriki wa siasa.”

”Vyam avya siasa vinawajibu wa kudumisha haki na usawa katika jamii zao kwakuwa wanawake ndio kundi kubwa la upigaji kura,” alisema

Kwa upande wake, Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Mussa Salum alianza kwa kuwashukuru Tamwa kwa kuwakutanisha viongozi wa dini ili kujadiliana kwa pamoja kuhusu masuala mbalimbali ya uchaguzi huo hususan nafasi ya mwanamke katika uongozi.

“Wanawake wanapaswa kuwa mstari wa mbele katika kugombea nafasi mbalimbali za uongozi na kutambua umuhimu wa kushika nafasi hizo za uongozi.”

“’Tunawahimiza wanawake kuwa mstari wa mbele katika kugombea nafasi mbalimbali za uongozi, sisi kamati ya viongozi wa dini, tunahimiza vyama vya siasa kutambua umuhimu na kuwapa nafasi wanawake kushiriki kugombea nafasi mbalimbali za uongozi,” alisema Sheikh Alhad.

Alisema wakati umefika sasa wanawake kupewa kipaumbele kushiriki kikamilifu kugombea nafasi za uongozi.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Gardner Habash wa Clouds Fm afariki dunia

Spread the loveALIYEKUWA mtangazaji wa kipindi cha Jahazi kinachorushwa na kituo cha...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Wauguzi, madaktari 1000 kugawiwa mitungi ya Oryx Gas

Spread the loveKAMPUNI ya Oryx Gas na Taasisi ya Doris Mollel Foundation...

Habari Mchanganyiko

Tanzania yachaguliwa Makamu wa Rais Tume ya Shirika la Hali ya Hewa Duniani

Spread the love  TANZANIA kupitia Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA)...

Habari Mchanganyiko

NEMC yaonya wanaojenga bila tathmini ya mazingira

Spread the loveBARAZA la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC),...

error: Content is protected !!