Friday , 29 March 2024
Home Habari Mchanganyiko Uchaguzi mkuu 2020: Vyombo vya habari Tanzania vyapewa somo
Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Uchaguzi mkuu 2020: Vyombo vya habari Tanzania vyapewa somo

Waandishi wa habari
Spread the love

VYOMBO vya habari nchini Tanzania, vimetakiwa kutoa uwiano sawa kwa wanawake na wanaume wakati wa kuhabarisha umma hasa kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba, 2020. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Hayo yamesemwa leo Jumatano tarehe 20 Mei, 2020 na Mtandao wa Wanawake, Katiba, Uchaguzi na Uongozi chini ya uratibu wa Mfuko wa Udhamini wa  Wanawake Tanzania (WFT) wakati ukitoa mrejesho wa uchambuzi wa sheria tano za uchaguzi kwa mrengo wa jinsia.

Malengo ya kuchambua sheria hizo ili kubainisha mapengo yaliyoko yanayoweza kuwa kikwazo kwa ushiriki wa wanawake kaika uongozi na kushirikisha wadau mbalimbali hususani wale wenye nia ya kutetea haki za wanawake za ushiriki katika uongozi.

Pia, kutoa mapendekezo mahususi yatakayoongoza wadau mbalimbali katika kuchukua hatua stahiki zenye kukabiliana na sheria za ubaguzi wa aina zote hususani ubaguzi wa jinsia

Mwenyekiti wa WFT, Profesa Ruth Meena akitoa uchambuzi huo mbele ya wanahabari kwa njia ya mtandao ‘video conference’ amesema wanahabari wanapaswa kujielimisha kuhusu masuala ya jinsia katika mchakato wote wa uchaguzi ili kubaini mapengo ya utekelezwaji wa sheria za uchaguzi kwa mrengo wa jinsia.

“Maarifa haya yatawapa wanahabari nyenzo ya kutetea haki ya ushiriki wa wanawake katika mchakato wa uchaguzi. Vyombo vya Habari vinahimizwa kutumia takwimu za chaguzi zilizopita kama nyenzo ya utetezi,” amesema Profesa Ruth

“Vilevile, vyombo vya habari tunavishauri kuandika makala mbalimbali na kutayarisha vipindi maalum vinavyolenga kuibua mjadala wa kitaifa kuhusu ushiriki wa wanawake katika mchakato wa uchaguzi,” amesema

Profesa Ruth amesema, vyombo vya habari, viwape wagombea wanawake kipaumbele kwenye matamko yao wakati wa kampeni na wanahabari watoe taarifa wakati wa kupiga kura utakapofika kuhusu vitendo vya wanawake kunyimwa haki ya kupiga na kupigiwa kura.

“Waandishi wa habari watafuta habari, watafuteni wanawake na hasa wale wenye kuonesha nia wawe chanzo cha habari, kuhakikisha habari  zinatoa  taswira chana ya wanawake wanaowania Kuhakiki matumizi ya lugha ili kuondoa zile lugha za kudhalilisha wanawake,  kushawishi wahariri watoe nafasi ya kwanza kwenye kurasa za mbele au kwenye vichwa vya habari,” amesema.

Mwenyekiti wa WFT, Profesa Ruth Meena

Profesa Ruth amesema, waandishi wa habari wanaapswa kutafuta habari, watafuteni wanawake na hasa wale wenye kuonesha nia wawe chanzo cha habari, kuhakikisha habari  zinatoa  taswira chana ya wanawake wanaowania.

“Kuhakiki matumizi ya lugha ili kuondoa zile lugha za kudhalilisha wanawake,” amesema

Sheria zilizochambuliwa ni:

  • Sheria ya  Taifa ya Uchaguzi Sura ya 343 ya 2015,
  • Sheria ya Uchaguzi ya Zanzibar namba 4  (2018)
  • Sheria ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa namba 4 ya mwaka 1979 s namba 292 kama ilivofanyiwa marekebisho mwaka 2010 na mwaka 2015)
  • Sheria ya  Serikali Za Mitaa ( Mamlaka za Wilaya Sura 287 kama ilivyorekebishwa 2002)
  • Sheria za Serikali za Mitaa za mmlaka za miji sura ya 288 na mamlaka za wilaya sura ya 287.
  • Pamoja na sheria hizi, uchambuzi wa  Katiba za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (1977) na ile ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar zikiwa sheria mama zinazoongoza utunzi wa sheria zote za nchi.

Profesa Ruth amesema, Tanzania ni miongoni mwa nchi zilizoingia mikataba mbalimbali ya kimataifa ya kupigania usawa wa kijinsia hivyo, kutoa wito kwa wanahabari kuwa nayo na kuisoma ili kupata uelewa wa kina wa hasa yapi yalikubaliwa.

Naye Mkurugenzi wa Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania (TAMWA), Rose Rouben amesema, vyombo vya habari vina nafasi kubwa ya kutetea usawa wa kijinsia katika maeneo mbalimbali ikiwemo kuonyesha mafanikio ya wanawake.

Rose amesema, kuna mambo yanafanywa na wanaume lakini hayaandikwi lakini hay ohayo yakifanywa na mwanamke, yanapewa kipaumbele jambo linalodidimisha jitihada za kupigania usawa wa kijinsia.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Nani anasema kuna hasara ATCL?

Spread the loveRIPOTI za makusanyo na matumizi ya fedha katika Kampuni ya...

Habari za SiasaTangulizi

CAG: Wastaafu, wenza wao chanzo NHIF kufilisika

Spread the loveRIPOTI ya ukaguzi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu...

Habari za SiasaTangulizi

Vikundi hewa 851 vyalamba bilioni 2.6 mikopo ya halmashauri

Spread the loveVIKUNDI hewa vya wajasirimali wadogo 851 kutoka katika halmashauri 19...

Habari za SiasaTangulizi

Mashirika matano yapata hasara mabilioni ya fedha

Spread the loveMASHIRIKA matano ya Serikali yanayojiendesha kibiashara, yamepata hasara ya mabilioni...

error: Content is protected !!