Uchaguzi Mkuu 2020: Takukuru yamtia mbaroni Aden Rage

Spread the love

TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) Mkoa wa Tabora nchini Tanzania, inamshikilia Ismail Aden Rage kwa tuhuma za rushwa na kuanza kampeni kabla ya wakati za uchaguzi mkuu wa Oktoba 2020. Anaripoti Mwandishi Wetu, Tabora … (endelea).

Rage alishikiliwa na Takukuru kuanzia tarehe 23 hadi 24 Mei, 2020 alipoachiwa kwa dhamana baada ya taasisi hiyo, kupokea taarifa kuwa Mkurugenzi huyo wa Voice of Tabora FM aliwakusanya viongozi wa kata na matawi wa CCM kwa lengo la kuwashawishi wampigie kura.

Taarifa ya Mussa Chaulo, Mkuu wa Takukuru Mkoa wa Tabora aliyoitoa leo Jumatatu tarehe 25 Mei, 2020 imesema uchunguzi wa suala hilo unaendelea.

Chaulo amewaonya wale wote walioanza kujipitisha ili kufanya ushawishi kwa wanachama ili wawachagua watachukuliwa hatua kali za kisheria.

Rage aliwahi kuwa mbunge wa Tabora Mjini kupitia CCM kati ya mwaka 2010 na 2015.

Pia, amewahi kuwa Rais wa klabu ya Simba ya Jijini Dar es Salaam

About Masalu Erasto

Leave a Reply

Your email address will not be published.

error: Content is protected !!