Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa

Uchaguzi Mkuu 2020: Majaliwa atoa maagizo kwa Takukuru

Spread the love

WAZIRI Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa amesema Serikali imewaagiza Makamanda wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) nchini wahakikishe wanawakamata na kuwachukulia hatua watu wote watakaojihusisha na vitendo vya rushwa kuelekea uchaguzi mkuu wa Oktoba 2020. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea).

“Watu wamezoea vitendo vya rushwa kwenye uchaguzi, Serikali tumeagiza kwa kamati za ulinzi na usalama zishirikiane kuhakikisha kwamba hakuna vitendo vya rushwa katika uchaguzi na yeyote ambaye anajihusisha na rushwa asiachwe,” amesema.

Alitoa kauli hiyo jana jioni Jumamosi, Juni 20, 2020 wakati akizungumza na viongozi wa mkoa wa Lindi mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Nachingwea akiwa njiani kuelekea wilayani Ruangwa kwa ziara ya kikazi.

Taarifa iliyotolewa na ofisi ya waziri mkuu ilimnukuu Majaliwa akisema, kitendo cha kutoa na kupokea rushwa ni kosa, hivyo viongozi hao wa TAKUKURU nchini hawana budi kuwachukulia hatua watu wote watakaobainika kujihusisha na vitendo hivyo.

Brigedia Jenerali, John Mbungo, Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru

Vilevile, Waziri Mkuu aliwataka Makamanda wa TAKUKURU katika wilaya zote nchini wahakikishe wanawakamata watu wote watakaojihusisha na vitendo vya rushwa wakiwemo na wapambe ambao ndio wachochezi wa vitendo hivyo.

Waziri Mkuu alitoa maagizo hayo ili kuhakikisha uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba mwaka huu unakuwa huru na wa haki, hivyo kuwawezesha wananchi kuchagua viongozi wanaowahitaji na si kwa msukumo wa rushwa.

Katika hotuba yake aliyoisoma Juni 15, 2020 bungeni jijini Dodoma wakati akihitimisha mkutano wa 19 wa Bunge, Waziri Mkuu aliwataka viongozi wa vyama vya siasa na wadau wengine wa uchaguzi wa

WAZIRI Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa amesema Serikali imewaagiza Makamanda wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) nchini wahakikishe wanawakamata na kuwachukulia hatua watu wote watakaojihusisha na vitendo vya rushwa kuelekea uchaguzi mkuu wa Oktoba 2020. Anaripoti Mwandishi Wetu...(endelea). “Watu wamezoea vitendo vya rushwa kwenye uchaguzi, Serikali tumeagiza kwa kamati za ulinzi na usalama zishirikiane kuhakikisha kwamba hakuna vitendo vya rushwa katika uchaguzi na yeyote ambaye anajihusisha na rushwa asiachwe," amesema. Alitoa kauli hiyo jana jioni Jumamosi, Juni 20, 2020 wakati akizungumza na viongozi wa mkoa wa Lindi mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Nachingwea…

Review Overview

User Rating: Be the first one !

About Mwandishi Wetu

Leave a Reply

Your email address will not be published.

error: Content is protected !!