Saturday , 20 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Uchaguzi mkuu 2020: Chadema yafungua milango ya ushirikiano
Habari za Siasa

Uchaguzi mkuu 2020: Chadema yafungua milango ya ushirikiano

Spread the love

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) nchini Tanzania, kimefungua milango ya majadiliano na vyama vingine vya upinzani ili kushirikiana katika uchaguzi mkuu wa Oktoba 2020. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Uamuzi wa chama hicho kikuu cha upinzani nchini humo, kimetangaza hatua hiyo ikiwa ni takribani miezi minne kabla ya kufanyika kwa uchaguzi huo unaoshirikisha vyama vingi vya siasa.

Katika uchaguzi mkuu uliopita wa tarehe 25 Oktoba 2020, Chadema ilishirikiana na vyama vitatu vya NCCR-Mageuzi, NLD na CUF na kuunda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa).

Umoja huo ulikubaliana kuachiana kata, majimbo na kumsimamisha mgombea urais mmoja ambaye alikuwa Edward Lowassa, waziri mkuu wa zamani wa Tanzania.

Leo Jumatano tarehe 3 Juni 2020, Katibu Mkuu wa Chadema, John Mnyika, akizungumza na waandishi wa habari makao makuu ya chama hicho, Kinondoni jijini Dar es Salaam amesema, “kuanzia leo, tumefungua milango ya majadiliano na vyama vingine vya siasa.”

“Tunafungua mlango wa majadiliano na vyama ambavyo vinadhamira ya kweli ya kushirikiana kuiondoa CCM madarakani,” amesema Mnyika.

Akijibu swali aliloulizwa na MwanaHALISI ONLINE kwamba ushirikiano wa mwaka 2015 uliounda Ukawa, hauna dalili kama mwaka huu utakuwapo, ni vyama gani na vingapi watashirikiana navyo, Mnyika amesema, muda ukifika watazungumza, lakini sasa wamefungua milango.

Ugumu wa Ukawa wa mwaka 2015 kuendelea na mwaka huu unatokana na mazingira ya kinachoendelea ndani ya NCCR-Mageuzi na CUF.

Katika siku za hivi karibuni, NCCR-Mageuzi kimekuwa kikiwapokea viongozi na wanachama wa vyama vya upizania hususan kutoka Chadema huku wakirusha tuhuma kwa Chadema na viongozi wake, jambo ambalo linakuwa na ugumu kushirikiana.

Baadhi ya waliotangaza kutimkia NCCR-Mageuzi ni wabunge; Anthony Komu (Moshi Vijijini), Joseph Selasini (Rombo), Susan Maselle na Joyce Sokombi ambao ni wabunge wa viti maalum.

Kwa pamoja, wamesema, watahamia NCCR)-Mageuzi baada ya Bunge la Tanzania kuvunjwa.

CUF ambayo mwaka 2015 ilikuwa ikiongozwa na Mwenyekiti, Profesa Ibrahim Lipumba ambaye baadaye alijizulu katikati ya uchaguzi na lakini alirejea tena uchaguzi ulipomalizika, jambo ambalo wachambuzi wa kisiasa wamekuwa wakiliona hilo ni doa kwa CUF kushirikiana na Chadema.

Duru za kisiasa, zimekuwa zikidokeza kwamba, pamoja na uwepo wa vyama vingine zaidi ya 16 vyenye usajili wa kudumu, kuna kila dalili za Chadema kushirikiana na ACT-Wazalendo katika uchaguzi huo.

Hii inapewa nguvu na ujumbe alioundika Zitto Kabwe, Kiongozi wa ACT-wazalendo katika ukurasa wake wa Twitter kwamba, kuelekea uchaguzi mkuu, inahitaji ushirikiano wa vyama viwili tu ambavyo ni Chadema na ACT-Wazalendo.

ACT-Wazalendo kimekuwa na nguvu hususan upande wa Zanzibar, baada ya kuwapokea waliokuwa wananchama na viongozi waandamizi kutoka Chama cha Wananchi (CUF) wakiongozwa na Maalim Seif Sharif Hamad.

Timu ya Maalim Seif ambaye kwa sasa ni mwenyekiti wa ACT-Wazalendo inajipanga kuelekea uchaguzi huo na mwaka 2015 akiwa CUF, aligombea urais wa Zanzibar na kutoa mchuano mkali.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Dk. Mwakyembe : Zanzibar waliongoza kutaka Serikali 2 za muungano

Spread the love  MWANASIASA mkongwe nchini, Dk. Harrison Mwakyembe, amesema mjadala wa...

Habari za SiasaTangulizi

Rais Samia ataja mikakati ya kufikia trilioni 2 biashara Uturuki, Tz

Spread the loveWakati Tanzania na Uturuki zikidhamiria kuongeza kiwango cha biashara hadi...

BiasharaHabari za Siasa

Mavunde aagiza Perseus kuharakisha fidia Sengerema

Spread the loveWaziri wa Madini, Anthony Mavunde ameipongeza Kampuni ya Perseus kwa...

Habari za Siasa

Kigogo Chadema awanyooshea vidole vigogo serikalini kuhusu ripoti ya CAG

Spread the love  MWANACHAMA wa Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Boniface Jacob, amedai...

error: Content is protected !!