Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) nchini Tanzania, Dk. Bashiru Ally

Uchaguzi Mkuu 2020: CCM yaanza mbwembwe

Spread the love

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) nchini Tanzania kimeanza kumwaga tambo, mbwembwe na kejeli dhidi ya vyama pinzania kuelekea uchaguzi mkuu wa Jumatano tarehe 28 Oktoba 2020. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea).

Dk. Bashiru Ally, Katibu Mkuu wa chama hicho akizungumza leo Alhamisi tarehe 6 Agosti 2020, Makao Makuu ya CCM, jijini Dodoma baada ya Dk. John Magufuli, mgombea urais kupitia chama hicho kuchukua fomu za kugombea urais amesema, safari hii chama hicho kitaongoza halmashauri zote nchini.

“Ushindi wa mwaka huu ni wa kishindo kikubwa, tutashinda nafasi za kutosha za udiwani, tutaongoza halmashauri zote nchi nzima, tutakuwa na wabunge wengi wa Bunge la Jamhuri.”

“Tutakuwa na wawakilishi wa kutosha katika Baraza la Wawakilishi Zanzibar, tutashinda urais wa Zanzibar mapema. Kwanini tuna uhakika huo, ni kwa sababu tumefanya kazi. Hatujafanya kazi na bata, tumefanya kazi na Watanzania. CCM si ya kufanya kazi na na bata, tena bata wachafu,” amesema Dk. Bashiru.

Msemo wa KaziNaBata umenzishwa na Chama cha ACT-Wazalendo, kikieleza kwamba mfanya kazi lazima apate muda wa ‘kula bara’ na sio Kazi Tu. Mwasisi wa msemo huo ni Zitto Kabwe, kiongozi wa chama hicho.

Dk. Bashiru amesema, Dk. Magufuli kafanya kazi na Watanzania na hao ndio watakaompigia kura za kumrejesha madarakani kwenye uchaguzi mkuu ujao.

“Uko msemo mwingine mtausikia, eta atapigiwa kura na umeme vijijini, shule, ndege, madaraja. Watu watakupigia kura kwasababu vitu hivyo umevifanya kwa jasho lao. Madaraja hayajijengi bali yanajengwa na Watanzania.

“Bila madaraja, reli, umemeo wa kutosha, elimu, chakula cha uhakika, afya, uslama na amani, upendo na mashikamano visipokuwepo, hakuna Tanzania,” amesema Dk. Bashiru.

Katibu Mkuu huyo amesema, Dk. Magufuli kwenye tawala wake, amekuwa akifuata nyayo za Hayati Mwalim Julius Nyerere ambaye alikuwa Rais wa Kwanza wa Tanzania.

“Umefanya kazi na watu, utapigiwa na watu na utaongoza watu. wewe sio mwenyekiti wa CCM wa kudumu, wala wewe sio rais wa kudumu. Unafuata nyayo za Mwalimu Nyerere.

“Kazi ya usultani wa vyama waachie wengine, kazi ya kubadilisha rangi za vyama waachie wengine. Chama Cha Mapinduzi ni chama cha ukombozi, kinashindana na vyama vya uchaguzi,” amesema.

Dk. Bashiru pia amepongeza hatua ya baadhi ya vyama vya upinzani kuamua kumuunga mkono mgombea urais wa chama hicho.

Miongoni vya viongozi wa vyama aliowataja ni Augustino Mrema, Mwenyekiti wa Chama cha TLP na John Momose Cheyo ambaye ni Mwenyekiti wa Chama cha UDP.

“Mzee Mrema ameona mbali, Cheyo ambaye anatuunga mkono ameona mbali, waliobaki waje, tuko tayari,” amesema Dk. Bashiru.

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) nchini Tanzania kimeanza kumwaga tambo, mbwembwe na kejeli dhidi ya vyama pinzania kuelekea uchaguzi mkuu wa Jumatano tarehe 28 Oktoba 2020. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea). Dk. Bashiru Ally, Katibu Mkuu wa chama hicho akizungumza leo Alhamisi tarehe 6 Agosti 2020, Makao Makuu ya CCM, jijini Dodoma baada ya Dk. John Magufuli, mgombea urais kupitia chama hicho kuchukua fomu za kugombea urais amesema, safari hii chama hicho kitaongoza halmashauri zote nchini. “Ushindi wa mwaka huu ni wa kishindo kikubwa, tutashinda nafasi za kutosha za udiwani, tutaongoza halmashauri zote nchi nzima, tutakuwa na wabunge wengi wa…

Review Overview

User Rating: Be the first one !

About Mwandishi Wetu

Leave a Reply

Your email address will not be published.

error: Content is protected !!