Thursday , 25 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Ubunge CCM: Angellah Akilimani ajitosa Ukonga
Habari za Siasa

Ubunge CCM: Angellah Akilimani ajitosa Ukonga

Spread the love

ANGELLAH Akilimali, Mkuu wa Idara ya siasa na habari wa vyombo vya habari vya Chama Cha Mapinduzi (CCM) amejitosa kuwania ubunge Ukonga. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam (endelea)

Angellah ambaye pia mwandishi wa habari mkongwe amechukua fomu Ofisi za CCM Wilaya ya Ilala leo Jumatano tarehe 15 Julai 2020 akiomba chama hicho kumpitisha kuwania ubunge jimbo la Ukonga jijini Dar es Salaam.

Mara baada ya kukabidhiwa fomu na Iddi Mkowa, Katibu wa CCM wilayani humo, Angella amesema, amejitosa kuomba ridhaa ya chama hicho ili kuwatumikia wana Ukonga.

“Kama mwanachama, nimetumia haki yangu kikatiba kuchukua fomu na nitarejesha na mwisho chama kitaendelea na mchakato utakapokamilika atapatikana mmoja,” amesema Angellah

Angellah amewahi kuwa kaimu mkurugenzi wa redio ya chama hicho redio Uhuru na Mjumbe wa Halmashauri Kuu CCM (NEC).

Kwa upande wake, Katibu wa CCM Wilaya ya Iddi Mkowa amesema Wilaya hiyo ina majimbo matatu ambapo hadi kufikia leo Jumatano saa 6 mchana, Ukonga wamejitokeza 85, Ilala 12 na Segerea 51.

Mkowa amewaomba wanachama wenye sifa za kuwania uongozi, waendelee kujitokeza.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Prof. Muhongo akomalia matumizi nishati jadidifu kuondoa uhaba wa umeme

Spread the love  MBUNGE wa Musoma Vijijini (CCM), Profesa Sospeter Muhongo, ameendelea...

Habari za Siasa

Kilosa yawa mfano wa kuigwa miradi ya Mwenge nchini

Spread the love  KIONGOZI wa Mbio za Mwenge Kitaifa Godfrey Mzava amezitaka...

Habari za SiasaTangulizi

Biteko ataja vipaumbele 7 bajeti nishati 2024/25

Spread the love  NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mwekezaji amwaga bil. 39 kujenga viwanda 3 vya uchenjuaji

Spread the loveKampuni ya Mineral Access System Limited (MAST) inayoiwakilishwa kampuni ya...

error: Content is protected !!