Thursday , 28 March 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Tuseme imetosha ufisadi huu mpya
Habari za Siasa

Tuseme imetosha ufisadi huu mpya

Valentino Mlowola, Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru
Spread the love

MWAKA 2018 moja ya mambo tunayotakiwa kuyapinga kama Watanzania ni hili la ufisadi unaofanywa na wanasiasa wanaohama vyama na kuachia nafasi zao za udiwani na ubunge. Anaandika Mwandishi Wetu …. (endelea).

Wanasaisa hao kila wanapohama vyama vyao wamekuwa wakijitetea kwa ngonjera za kitoto kwamba wanafanya hivyo kwa sababu wanaunga mkono juhudi za serikali katika mipango na mikakati mbalimbali ya kuwaletea maendeleo Watanzania.

Ingawa ni haki yao kuhama na hakuna sheria inayowazuia kufanya hivyo, lakini kuna haja serikali hii inayojipambanua kupamabana na ufisadi iwaone hawa watu kama mafisadi wapya.

Huu ni ufisadi mpya kabisa ambao unazidi kuongezeka kila kukicha ingawa siku za nyuma ulikuwapo, lakini kwa sasa umekuja kwa njia nyingine.

Wanasiasa hawa wanaohama vyama vya upinzani na kujiunga na Chama Cha Mapinduzi (CCM) na wale wanotoka CCM na kujiunga na upinzani wote wana makosa makubwa ambayo yanafanana.

Kitendo cha wanasiasa hawa kuhama vyama vyao na kuachia nafasi zao siyo tatizo kwa Watanzania, lakini tatizo linakuja pale serikali kupitia Tume ya Tiafa ya Uchaguzi (NEC), inapolazimika kuitisha uchaguzi mwingine kwa kutumia fedha za walipa kodi.

Gharama za kuandaa uchaguzi mmoja wa diwani zinakadiriwa kufikia Sh. 250 milioni na kwa mbunge zinadaiwa kufikia shilingi bilioni tatu.

Fedha hizi za kuandaa uchaguzi wa udiwani zinazweza kutosha kuchimba visima virefu vya maji vinavyofikia 25 kwa gharama ya Sh. milioni 10 kwa kisiama kimoja ambavyo vinaweza kutosheleza maji kwa Kata nzima.

Kwa upande wa gharama za kuitisha uchaguzi kwa jimbo moja nazo zinaweza kutosha kutoa huduma ya maji kwa jimbo zima na hivyo kumaliza kero hiyo.

Kwa bahati mbaya hili linaonekana kama ni jambo la kawaida na wanasiasa wanasema katika kutafuta demokrasia suala la gharama haliangaliwi.

Swali la kujiuliza ni je? hawa watu hivi ni kweli wanaunga mkono juhudi za serikali katika kuwaletea wananchi maendeleo ama wanasababisha ufisadi?

Kuna haja kwa serikali kuliangalia suala hili kwa umakini, badala ya kulichukulia kisiasa kwa kuwa huu ni ufisadi mpya.

Kuna mambo mengi yanayozuiwa na serikali yasifanyike hata kama yapo kwa mujibu wa sheria ikiwamo kuzuia mikutano ya vyama vya siasa.

Kwa hiyo naamini hata hili la madiwani na wabunge kuhama vyama na kuachia nafasi zao, kuna haja ya serikali kulizuia japo sheria haiwakatazi wao kuhama.

Kuna njia moja tu ya kakataa hili ikiwamo NEC kuliacha wazi jimbo ama kata mpaka miaka mitano ipite baada ya kufanyika uchaguzi mkuu.

Hili janga ni kubwa ambalo kwa sasa linaanza kuonekana kama ni ushujaa pale mwanasiasa anapohama chama kimoja na kuachia nafasi yake aliyokabidhiwa katika uchaguzi mkuu ambao hufanyika kila bada ya miaka mitano kupita.

Huu ni ufisadi mbaya ambao kwa bahati mbaya umekuwa ukipigiwa makofi bila kujua fedha za walipa kodi ndizo zitakazotumika kuandaa uchaguzi mwingine.

Katika hali isiyofuarahisha wanasiasa hawa wamesikika wakisema baadhi yao kwamba wanaachia nafasi zao ili kuunga mkono serikali iliyopo madarakani kwa madai kwamba tangu iwepo imekuwa ikifanya mambo mazuri.

Kwa wale wanaotoka CCM wao wamekuwa wakitamka bayana wametoka huko kwa hiari yao na kujiunga na upinzani huku wakisisitiza kwamba wanayo haki ya kuhama chama chochote na kujiunga na kile wanachokitaka.

Moja ya kazi ya mbunge ni kuisimamia na kuishauri serikali, sasa inapotokea amehama chama na kusababisha hasara kubwa niliyoitaja hapo juu, anawezaje kusema amehama ili kuunga mkono juhudi za serikali?

Hata hivyo, CCM inadai kwamba hii ni mbinu mpya za kimkakati kulingana na kasi ya dunia na mahitaji ya jamii, ndizo zinazowarudisha wapinzani katika chama hicho tawala.

Kauli hiyo iliwahi kutolewa na Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM anayehusika na siasa na uhusiano wa kimataifa, Kanali Ngemela Lubinga wakati akizungumza na wanahabari mjini Moshi.

Kanali Lubinga alisema hata madiwani wa Chadema katika jimbo la Arumeru waliojiuzulu na kumuunga mkono Rais Magufuli walifanya hivyo kutokana na kuridhishwa na utendaji kazi wa Serikali.

“Hii sasa hivi ni CCM mpya na Tanzania mpya. CCM tulijifanyia tathmini ya miaka 40 na kuona mapungufu na tumeyarekebisha ndani ya CCM na serikalini. Kasi hii inawavutia wengi,” alisema.

“Tumeanzisha mbinu mpya za kimkakati kulingana na hitaji la jamii. Dunia inakwenda spidi na spidi ya dunia inavyokwenda lazima chama tawala kiendane na spidi hiyo na hitaji la jamii,” alisisitiza.

Pamoja na yote haya kuna haja ya kutafuta njia bora ya kumaliza ufisadi huu mpya ambao kwa bahati mbaya unafanywa na wanasiasa lakini unashangiliwa huku ukigharimu fedha za walipa kodi.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Nani anasema kuna hasara ATCL?

Spread the loveRIPOTI za makusanyo na matumizi ya fedha katika Kampuni ya...

Habari za SiasaTangulizi

CAG: Wastaafu, wenza wao chanzo NHIF kufilisika

Spread the loveRIPOTI ya ukaguzi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu...

Habari za SiasaTangulizi

Vikundi hewa 851 vyalamba bilioni 2.6 mikopo ya halmashauri

Spread the loveVIKUNDI hewa vya wajasirimali wadogo 851 kutoka katika halmashauri 19...

Habari za SiasaTangulizi

Mashirika matano yapata hasara mabilioni ya fedha

Spread the loveMASHIRIKA matano ya Serikali yanayojiendesha kibiashara, yamepata hasara ya mabilioni...

error: Content is protected !!