Saturday , 20 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Tundu Lissu kuanika kilichompata
Habari za SiasaTangulizi

Tundu Lissu kuanika kilichompata

Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa Chadema akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) juu ya afya ya Tundu Lissu (picha ndogo)
Spread the love

AFYA ya Mbunge wa Singida Mashariki (Chadema), Tundu Lissu anayetibiwa majeraha ya risasi kwenye hospitali kuu ya Nairobi, inaendelea kuimarika na kwamba muda si mrefu ataanza kuzungumza na wananchi kupitia mkanda wa video, anaandika Faki Sosi.

Hayo yameeleza jijini Dar es Salaam leo Jumanne na mwenyekiti wa taifa wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe, katika mkutano wake na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.

“Afya ya mheshimiwa Lissu inazidi kuimarika na muda wowote kunzia leo ataanza kuzungumza kupitia video ambazo zitarushwa katika mitandao ya kijamii,” ameeleza Mbowe.

Amesema, Lissu anatarajiwa kuanza kuzungumza na video yake ya kwanza inatarajiwa kuonekana katika mitandao mbalimbali ya kijamii ili kuwatia moyo watu wote waliomuombea na kumtia moyo.

Amesema, tayari Lissu ameimarika vya kutosha na kuanza kujitambua na sasa ana uwezo wa kuzungumza na amepanga kusema neno kwa Watanzania wenzake juu ya afya yake.

Mbowe amesema yeye na wenzake ndani ya Chadema, hawapo tayari kufa, hawatakiri umauti, hawatarudi nyuma pamoja na kujua hatari kubwa iliyo mbele yao.

Akizungumzia gharama za matibabu, Mbowe ambaye ni mbunge wa Hai na kiongozi wa upinzani bungeni amesema, hadi sasa wameshatumia mamilioni ya shilingi kugharamia matibabu ya Lissu.

“Huwezi kumsemea mtu akiwa na akili timamu. Sisi kama chama tulijipa jukumu la kumsemea Lissu kila jambo wakati alipokuwa kwenye hali mbaya. Lakini sasa ameimarika vya kutosha na siyo siri kuanzia leo, tutaanza kutoa picha zake,” ameeleza Mbowe.

Wakati huo huo, Mbowe amesisitiza kufanyika uchunguzi huru wa shambulio la Lissu ambapo ameeleza kuwa kuna umuhimu vyombo vya nje vya uchunguzi vifanye kazi hiyo ili kupata ukweli.

Amesema, “hii haitakuwa mara kwanza watu wa Scotlandyad kuja kufanya uchunguzi….. moto uliochoma benki kuu ya Tanzania (BoT) mwaka 1984 ulichunguzi wake ulifanywa na Scotlandyad. Mashushu hawa kutoka Uengereza walifanya kazi hiyo kwa maombi ya serikali.”

Amesema, serikali ikiridhia wachunguzi hao wenye weredi kuingia nchini na kuchunguza tukio hilo, ukweli wa shambulio hilo ungepatikana.

Kuhusu dereva wa Lissu, anayefahamika kwa Simon Adam, Mbowe amesema, amekumbwa na tatizo la kisaikologia, hivyo anahitaji matibabu. Amesema, hafahamu muda ambao utakaotumika kukidhi matibabu yake, ingawa kwa maoni yake, “yanahitaji muda mrefu.”

Akijibu madai ya Jeshi la Polisi la kumtafuta dereva huyo kwa ajili ya mahojiano, Mbowe amesema, ‘kama polisi wananamtaka wamfuate Nairob.”

Amesema kuwa suala la matibabu ya Lissu linahisia kali za kisiasa kutokana na Bunge kutaka kumtibu kwenye mazingira ambayo wameweka fedha mbele kuliko uhai.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Rais Samia ataja mikakati ya kufikia trilioni 2 biashara Uturuki, Tz

Spread the loveWakati Tanzania na Uturuki zikidhamiria kuongeza kiwango cha biashara hadi...

BiasharaHabari za Siasa

Mavunde aagiza Perseus kuharakisha fidia Sengerema

Spread the loveWaziri wa Madini, Anthony Mavunde ameipongeza Kampuni ya Perseus kwa...

Habari za Siasa

Kigogo Chadema awanyooshea vidole vigogo serikalini kuhusu ripoti ya CAG

Spread the love  MWANACHAMA wa Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Boniface Jacob, amedai...

Habari za Siasa

Wabunge waikalia kooni TAKUKURU Bungeni

Spread the love  BAADHI ya wabunge wamelia na changamoto za utendaji wa...

error: Content is protected !!