Friday , 29 March 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Tundu Lissu azungumzia ushindi wa Dk. Magufuli
Habari za Siasa

Tundu Lissu azungumzia ushindi wa Dk. Magufuli

Tundu Lissu, Makamu Mwenyekiti Chadema
Spread the love

ALIYEKUWA Mgombea Urais wa Tanzania kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Tundu Lissu amezungumzia ushindi wa Mgombea wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. John Magufuli katika Uchaguzi Mkuu uliofanyika tarehe 28 Oktoba 2020 na kusema aliyajua mapema. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Jana tarehe 30 Oktoba 2020 Tume ya Taifa ya Uchaguzi Tanzania (NEC) ilimtangaza Dk.  Magufuli kuwa Rais mteule wa Tanzania, baada ya kupata kura milioni 12.5 kati ya milioni 15.9 zilizopigwa huku Lissu akipata kura milioni 1.9.

Akizungumzia matokeo hayo, Lissu amesema aliyatambua mapema. Huku akisistiza kuwa matokeo hayo hayakuwa halali kutokana na dosari zilizojitokeza kwenye uchaguzi huo.

“Magufuli hajashinda uchaguzi huu. Unakumbuka katika mkutano wangu wa kampeni tulisema kwamba tulikuwa na taarifa ya kwamba kulikuwa na kura za Magufuli na nilitamka ni milioni 12 na kura ambazo tume imezitangaza za Magufuli amepata ni milioni 12.5,” amesema Lissu.

Rais John Magufuli

Lissu amesema ushindi huo una dosari kwa madai kuwa matokeo yake yamesababisha Taifa kuwa na dalili za msiba kila mahali badala ya furaha na shamrashamra za ushindi.

“Walioshinda uchaguzi wa haki si huwa wanashangalia lakini kwa nini kuna dalili ya msiba? Kila mahali msiba wa Taifa sababu kila mtu anajua kwamba ushindi haukuwa wa haki,” amesema Lissu.

Wakati huo huo, Chadema na Chama cha A T-Wazalendo vimetangaza kutotambua matokeo ya uchaguzi huo, yaliyokipa ushindi wa kishindo wa CCM.

38 Comments

  • Lisu kama Umetumwa na Mume zako uje kuvuruga amani. Umekwama…wapelekee hilo lisamaki wakaendelee kulitafuna waingize hadi Pumbu..ila sio kuchezea amani yetu.

  • Lisu acha upumbavu huo, mandamano? Chukua mkewako na watoto zako mkaandamane na sio sisi

  • napenda MZEE wangu magufuli aongoze miaka 20 najua atakae kuja ato isogeza nchi kama alipo ifikisha rais magufuli sasa

  • Magufuli oyeee!
    Mungu akutangulie unapokamilisha awamu ya pili mitano tena Mkuu. Usikubali kutumikishwa longer than the period you deserve, your honour will be on legacy you created during your service tenure and the strong desire to serve the nation.
    I recommend you to ensure a great successor of your leadership.

  • Napenda kuwajulisha mnaopenda kukoment upuuzi ambao hauko kaa kimya Kama huna la maana. Mnamhukumu nini Lisu. Kama ameshinda Rais wetu Magufuli halina shida pia ni sawa kwani kafanya kazi na imeonekana kaleta maendeleo na yameonekana so just cool down uone kinachoendelea. Mimi mwenyewe Nampenda Rais wangu Magu Sana.

    Tatizo lenu watanzania mnapenda ushadadi ambao hauna maana. Swala la kusema kumtukana mtu Hilo si sahihi. Rais Magufuli ndie angestahili atukane wewe kinakuhusu nini. Wachani upuuzi ninyi watanzania Kama unaweza kukaa kimya kaa. Sipendi kuingia kwenye mtandao Ila nimesema acheni viongozi wafanye kazi mungu aliyowapa.

  • Naumia sana kuona kiongozi unaitisha watu kuandamana, huu ni muda kujenga taifa letu, na sio muda wa kuandamana, wanasiasa wengi wa kiafrica hawana uvumilivu wa kisiasa. Hawa watu hawatutakii mema kabisa, wanataka watu waandamane alfu yaanze kutokea mambo kama tunayoona Nigeria au.
    #Hatuandamani #TumeridhikaNaMatokeo

  • Uchaguzi umeisha,Tundu Lisu anayo haki ya kishera kuridhika au kutoridhishwa na matokeo na hatupaswi kumhukumu.Vyombo husika vipo kushughulikia malalamiko atakapopeleka!

  • Mimi nadhani sasa ni wakati mzuri was viongozi was upinzani kujitathmini na kujua wapi wslipokosea. Kilagpmbea aliyeshindwa ajiulize kwa makini kabisa kwa mini ameshindwa safari hii? Wapi alikosea? Na mini kipanyike ili next time arudi kwa kishindo kikubwa zaidi. Mungu ibariki Tanzania.

  • Sasa kama ulijua mapema si ungeacha hata kampeni, ila una ufunuo ulijua mapema magufuli atashinda kwa zaidi ya kura milioni 12 ndio maana ukajihami kwa kusema kuna kura milioni 12 zimeandaliwa. Anyway najua soon utarudi kwenu.

  • Kilio cha Watanzania kwa sasa ni mitandao ya kijamii, uchaguzi umeisha kwanini isifunguliwe? kuna watu wanaitegemea kwa shughuli zao za kiuchumi

  • Wewe unaesema lissu ana haki ya kuridhika au la, sidhani amewahi kunyimwa hiyo haki, tangia lini lissu ninaemjua mm akaridhika, shida yake ubinafsi mwingi wa kupitiliza na sidhali kwa umri wake anaeza kuwa mzalendo kama nimesema vibaya mungu anisamehe, kama ameshimdwa kuwa myenyekevu kwa fulsa aliyopata. Hatukaki kiongozi style yake Tanzania hii

  • Imagine kwenye kampain zake zote anatukana raisi na kudhihaki kazi aliyoifanya, kiongozi mwenye kichwa kizuri ni mpole na mwenye busara lakini siyo lissu, zito, mbowe ninaowajua mungu awalinde siwaombei mabaya ila natama wapate kofi la roho mtakatifu kama mtakatifu Paulo

  • Tangia lini ss tukaratibu uchaguzi wao hao akina lisu na wenzake wanaowasemea kuingilia matokeo jumuia ya Afrika mashariki na wengine wenye mapenzi mema wanatosha na so vinginevyo. Kwani moja ya majirani akipata shida wote twaumia kwa njia mbali mbali lkn akifanikiwa jirani wote twafaidika kwa njia mbali mbali. Jameni tuwe na mtazamo mpana

  • Lissu kuwa na uchu wa madaraka si kushindana epuka kwenda na majibu yako kwenye uwanja wa mjadala

  • HILO domo KAMA MKUNDU wa NYANI..! kama umepewa hela uje kuiweka nchi rehani..NENDA KABANDULIWE au rudisha hela za wabelgiji..SERA ZAKO ZA USHOGA zimefeli..kageuzwe na Ukoo wako sio Watz wenye akili timamu.

  • We shouldn’t insult other for what happened, ushindi wa Dr Magufuli. If you think that u can’t control your big mouth just keep quite! We are all Tanzanuans and we must respect.eacb other!

  • Tuponye majeraha kwa nguvu ya maridhiano ya pande mbili, ili tuwe na Taifa linalotunzwa kwa misingi ya Uhuru, haki na amani, tusitukane MTU tukifikiri ni MTU mmoja hapana tujue tunatukana watu walio nyuma yake (jamii ya watanzania wanaomkubali) kwa hiyo matusi yanaumiza wengi tunakuwa na taifa LA majeraha mengi….amani hutoweka kidogo kidogo mwisho hujaza kibaba, matusi ni wembe TCRA wameshauri Sana hili.

  • Sababu za Lisu kuwa Rais wetu kipenzi, Mzee wa hapa kazi tu, hazina mashiko, kwani anapodai kuwa kura 12m ni za kupanga ni none sense, mana ingekuwa kura za Magu 12m zinatofautiana sana na zile za majimboni angalau tungesema inakaribia na ukweli, lkn kura za majimbo na za Magu zinalingana kuonesha wa Tanzania wamekipigia chama cha mapinduzi, zilobaki ni kashfa za sungura alozikosa zabibu

  • Tundulisu na mashoga….nendeni ulaya mkaishi huko…hapa👇 Tanzania 🇹🇿 hatutaki vurugu🔥

  • Lissu hayo ni maamzi ya watz anguko lenu lilishatabiliwa lkn nyie hamkushtuka uwez kupiga kampeni kwa kuponda ujenz wa hosp unaponda ujenzi wa reli ujenzi wa madaraja ujenzi wa barabara ujenzi wa miundombinu ya umeme ukategemea mtz mweny akili atakupa kura maana unaonekana ni jinc gani ukipewa nchi hutafanya chochote yaani wew sera zako ni haki na uhuru wakati hvyo vitu watu wanavyo , njoo na sera zitakazowavutia watu utapata kura sa hv kapige kazi zingine

  • Lucy,tutolee uvivu maana naona unawatisha watu kisa wametoa mawazo yao.Pili,kwa mjibu wa sheria za tume na sheria za katiba ya jamhuri ya muungano wa Tanzania jpm kashinda kihalali.
    Huyu lisu kama anaona ameibiwa kura afate taratibu na sheria za nchi zinavyosema na si kutushawishi vijana kuingia barabarani heti tuandamane,au atuonyeshe mfano yy atangulize mke wake na ndugu zake mbele nasi tutafata

  • Achen kutoa matusi maan ushindi sawa waanzania mnao but subirin nn kinaendelea, usikute unauchonga mdomo tu kumbe tangu magu aingie madarakan unakula mlo mmoja!! Achen kufata mkumbo ishi kama mimi bendera fata upepo!! Sikilizia uone je hutojutia maamuz yako uloyafanya siku ya kupiga kura!! Achenkutukana!!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Chadema: Samia aunde tume kuchunguza mauaji mgodi wa Barick

Spread the loveRAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, ameombwa aunde tume huru kwa...

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Nani anasema kuna hasara ATCL?

Spread the loveRIPOTI za makusanyo na matumizi ya fedha katika Kampuni ya...

Habari za SiasaTangulizi

CAG: Wastaafu, wenza wao chanzo NHIF kufilisika

Spread the loveRIPOTI ya ukaguzi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu...

Habari za SiasaTangulizi

Vikundi hewa 851 vyalamba bilioni 2.6 mikopo ya halmashauri

Spread the loveVIKUNDI hewa vya wajasirimali wadogo 851 kutoka katika halmashauri 19...

error: Content is protected !!