Friday , 29 March 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Tundu Lissu ateuliwa kugombea urais Tanzania
Habari za SiasaTangulizi

Tundu Lissu ateuliwa kugombea urais Tanzania

Spread the love

TUME ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), imemteua Tundu Lisuu kuwa mgombea urais wa Tanzania kupitia Chadema na mgombea mwenza, Salum Mwalimu katika Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Jumatano 28 Oktoba 2020. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea).

Lissu na Mwalimu, wameteuliwa leo Jumanne tarehe 25 Agosti 2020 na Mwenyekiti wa NEC, Jaji Semistocles Kaijage baada ya kuwasili ofisi za tume hiyo jijini Dodoma.

Lissu ambaye ni Makamu Mwenyekiti wa Chadema, Bara amekuwa mgombea wa 15 kuteuliwa kuwania nafasi hiyo kupeperusha bendera ya Chadema kwenye uchaguzi huo unaoshirikisha vyama vingi.

Wengine walioteuliwa ni; John Pombe Magufuli (CCM), Leopard Mahona (NRA), John Shibuda (Ada Tadea), Mutamwega Mgaiwa (SAU), Cecilia Augustino Mwanga (Demokrasia Makini), Yeremia Maganja (NCCR-Mageuzi) na Profesa Ibrahim Lipumba wa CUF.

Pia wamo, Philip John Fumbo (DP), Bernard Membe (ACT- Wazalendo), Qeen Cuthbert Sendiga (ADC), Twalib Ibrahim Kadege (UPDP), Hashimu Rungwe (Chaumma), Khalfan Mohamed Mazurui (UMD) na Seif Maalim Seif (AAFP).

Baada ya kuhitimisha kwa uteuzi kwa wagombea hao, kutakuwa na muda wa uwekaji mapingamizi kwa mujibu wa sharia na mwisho ni kesho tarehe 26 Agosti 2020 saa 10 jioni.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Nani anasema kuna hasara ATCL?

Spread the loveRIPOTI za makusanyo na matumizi ya fedha katika Kampuni ya...

Habari za SiasaTangulizi

CAG: Wastaafu, wenza wao chanzo NHIF kufilisika

Spread the loveRIPOTI ya ukaguzi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu...

Habari za SiasaTangulizi

Vikundi hewa 851 vyalamba bilioni 2.6 mikopo ya halmashauri

Spread the loveVIKUNDI hewa vya wajasirimali wadogo 851 kutoka katika halmashauri 19...

Habari za SiasaTangulizi

Mashirika matano yapata hasara mabilioni ya fedha

Spread the loveMASHIRIKA matano ya Serikali yanayojiendesha kibiashara, yamepata hasara ya mabilioni...

error: Content is protected !!