Tuesday , 23 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Tundu Lissu aomba hifadhi Ujerumani
Habari za SiasaTangulizi

Tundu Lissu aomba hifadhi Ujerumani

Tundu Lissu, Makamu Mwenyekiti Chadema
Spread the love

ALIYEKUWA mgombea urais wa Chadema, katika uchaguzi mkuu uliyopita nchini Tanzania, Tundu Antipas Lissu, amekimbilia nyumbani kwa balozi wa Ujerumani, jijini Dar es Salaam, “kuomba hifadhi ya maisha yake.” Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).

Taarifa kutoka kwa watu waliokaribu na kiongozi huyo zinasema, Lissu pamoja na baadhi ya wasaidizi wake, wapo nyumbani kwa balozi huyo, kufuatia kupokea vitisho lukuki vinavyolenga kuondoa uhai wake.

Lissu na baadhi ya wasaidizi wake, wamekuwa nyumbani kwa balozi wa Ujerumani, nchini Tanzania, tokea Jumatano iliyopita ya tarehe 4 Novemba, 2020.

Akizungumza na MwanaHALISI Online, jana Alhamisi, Lissu amethibitisha kuwapo nyumbani kwa balozi huyo, na kwamba atakuwapo hapo hadi atakapohakikishiwa usalama wa maisha yake.

“Ni kweli kwamba niko nyumbani kwa balozi. Nimekuja kuomba hifadhi, ili kunusuru maisha yangu,” alieleza Lissu na kuongeza, kuondoka nyumbani kwa balozi huyo au kuendelea kuwapo kutategemea, hakikisho la usalama wake.

Msemaji wa Jeshi la Polisi Tanzania, David Misime

Alipoulizwa vitisho hivyo alianza kuvipokea lini, Lissu alisema, “nilianza kupokea vitisho vya maisha yangu, mara baada ya uchaguzi mkuu uliofanyika tarehe 28 Oktoba 2020.”

Amesema, “baada ya vitisho kuzidi kuongezeka, nilitafakari kwa kina taarifa za vitisho hivyo, pamoja na taarifa kutoka kwa ‘wasamaria wema, ndipo nilipoamua kwenda kutafuta hifadhi ya muda sehemu nyingine tofauti na nyumbani kwangu.”

Taarifa zinasema, ikiwa Lissu ambaye ni makamu mwenyekiti wa Chadema (Bara), atashindwa kuhakikishiwa usalama wake na vitisho hivyo vitaendelea, anaweza kufikiria kuondoka nchini kwa muda.

Kwa mujibu wa taarifa hizo, Lissu anapanga kuelekea nchini Ujerumani kwa ajili ya kutafuta hifadhi ya maisha yake na kujipanga upya kisiasa.

Lakini Msemaji wa jeshi la polisi nchini Tanzania, Kamishena Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP), David Misime, ameliambia MwanaHALISI Online kuwa jeshi lake, halina taarifa zozote kuhusu madai kuwa maisha ya Lissu yako hatarini.

Amesema, “jeshi linazungumzia kitu ambacho inakifahamu. Jeshi linazungumzia kitu ambacho kimetolewa taarifa. Hatuwezi kuzungumzia kitu ambacho, hakijatufikia. Hizo taarifa hatuna.”

Ameongeza, “hizo taarifa amezitoa lini? Sasa ungemuuliza yeye, maisha yake kama yako hatarini, ameripoti katika vyombo vya dola?

Kupatikana kwa taarifa kuwa maisha ya mwanasiasa huyo machachari wa upinzani nchini Tanzania yako hatarini, kunakuja miaka mitatu, tangu aliposhambuliwa kwa risasi na wanaoitwa, “watu wasiojulikana,” nyumbani kwake Area D, mjini Dodoma.

Shambulio dhidi ya Lissu, lilifanyika mchana wa tarehe 7 Septemba 2017, wakati alipokuwa akirejea nyumbani, akitokea kwenye viwanja vya Bunge, kuhudhuria mkutano wa bunge la asubuhi.

Mara baada ya tukio hilo ambalo lilimjeruhi vibaya, mbunge huyo wa zamani wa Singida Mashariki (Chadema), alisafirishwa hadi nchini Kenya kwa matibabu zaidi na baadaye nchini Ubelgiji.

Lissu alirejea nchini Jumatatu, tarehe 27 Julai 2020, kutokea nchini Ubelgiji na kujitumbukiza moja kwa moja kwenye kinyang’anyiro cha urais wa Tanzania.

Katika uchaguzi huo, Lissu alitangazwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), kushika nafasi ya pili kwa kupata kura 1.9 milioni, huku Rais John Pombe Magufuli wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), akitangazwa mshindi kwa kupata kura 12 milioni kati kura 15 milioni zilizopigwa.

Kwa upande wake, mshauri wa Lissu, Askofu Mkuu wa Kanisa la Moravian la Uamsho Tanzania na Mwenyekiti Mwenza wa Umoja wa Makanisa ya Moravian ya Uamsho duniani, Emmaus Bandekile Mwamakula, amedai kuwa “maisha ya Lissu yako hatarini.”

Askofu Mwamakula amesema, ameongea na Lissu na baada ya kushauriana kwa kina, wamekubaliana kuomba hifadhi kwenye ubalozi huo.

Alisema, Lissu alikwenda ubalozi wa Ujerumani (Umoja House) tarehe 3 Novemba na akiwa nje ya ubalozi huo, kusubiri taratibu, Polisi walimkamata na kumpeleka makao makuu ya polisi, jijini Dar es Salaam.

Alihojiwa kwa takribani dakika 15 akituhumiwa kuitisha maandamano ya amani yaliyolenga kupinga matokeo ya uchaguzi mkuu wa 28 Oktoba 2020, kinyume na kile kinachoitwa na polisi, “sheria za nchi.”

Anasema, “baada ya kutafakari kwa kina kuhusu hali halisi ya usalama wake katika mazingira ya sasa na baada ya kushauriana na wadau mbalimbali, imeonekana ni vema na ni hekima, Lissu kuendelea kuishi uhamishoni katika Ubalozi wa Ujerumani jijini Dar es Salaam hadi pale itakapoamriwa tena hapo baadaye.”

Askofu Mwamakula amesema, wanatoa wito kwa “watu wote walio nyuma ya mpango wa kutishia usalama wa maisha ya Lissu kwa kuelekeza, kufadhili, kutuma au kutekeleza mpango huo, kuacha mara moja kwa kuwa mkono wa Mungu na ulinzi wake upo pamoja na watu wasiokuwa na hatia.”

Baba Askofu Mwamakula anasisitiza hoa yake kwa kutumia maandiko matakatifu, akirejea Zaburi 35 na 121, pamoja na Ezekieli 33:1-20, kwamba kufanya hivyo, ni kutenda uovu.

Wakati Askofu Mwamakula anaeleza hayo, Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa anasema, jalada la tuhuma zinazomkabili Lissu na wenzake wawili, limepelekwa kwa mwendesha mashtaka wa Serikali kwa hatua zaidi.

32 Comments

  • Kwanini asikimbilie kwa wananchi wake badala ya kuwaangukia mabalozi?
    Ujue kwamba hawa mabalozi wana maslahi yao ya kisiasa na kiuchumi. Hawajali haki za binadamu. Ona jinsi balozi wa Marekani alivyokimbia Dodoma kumpongeza JPM
    Wao siku zote husema “We have no permanent friend, only permanent interest”
    Hizo risala zao za kukosoa uchaguzi ni kiini macho tu
    MAALIM SEIF NA TUNDU LISSU NA ZITTO KABWE NENDENI KWA WANANCHI SIO KWA MABALOZI !!!

  • Wananchi wana mamlaka gani? Katiba haina nafasi kwa wananchi.
    Nguvu zote amepewa Rais na vikaragosi wake. Ubinafsi wetu umeichuuza haki.yetu kwa serikali ovu inayodiriki kutowapa watu mgao wao wa keki ya taifa kwa vile walipiga kura kwa uhuru!!
    Lissu nenda penye salama yako. Na Mungu akulinde 2025 utuongoze ktk haki na kweli

  • LISSU mdogoangu MPIGANAJI na kiongozi wangu mahiri. Milele kaa mahali penye salama yako, hao wanaosema hujariport vitisho ndio walewale walokalia reports zako za vitisho mnamo July August na September 2017. Misiime mnafiki tu.

  • Sasa huyu angepata urais si ndo angewakabidhi hao wazungu kila kitu. Kama ana hofu kwanini aligombea? Angebaki ubelgiji kwa mitume wake

  • Anajidai kwamba hujariport utafikiri hata wanafnya chochote hata ukitepot?
    Mbona 2017 July August na September uliporeport hawajafanya lolote hadi ukapigwa risasi 38?? Huu ni mpango wao huu.
    Na kama wasingekuwa wanahusika wao magufuli anashindwa nini kuongea neno hata moja kumhusu LISSU na madhila yaliyompata? Magufuli ndiye muo…

  • Urais siyo baba wa familia,hivyo ni mchakato wa muda mrefu,vyama pinzani vinahitaji urais pasipo kuonesha jitihada yeyote kimaendeleo,labda wabadili mbinu kiutendaji,la sivyo ……… thanks

  • …ngoza huu uovu.
    Na ole wako magufuli LISSU apate tena misukosuko Kama hujaja kunyakuliwa hapo mithili ya kuku kunyakuliwa na mwewe ukaenda ICC

  • Naona kujitetea kwingi ndio mipango Mazima.ukiwa na watu wanaowahusudu wazungu bado unakuwa na fikra tegemezi.kwani hifadhi haipatikani katika nchi za kiafrika mpaka ulaya?mwisho WA siku wananchi wanakuwa na mashaka nawe kwasababu wanahisi unaweza kuwa umepangwa kuwa kibaraka WA wazungu ambao wamekupa hizo hifadhi.

  • Hatuna tume huru ya uchaguzi. Nawapongeza ambao hawa kupiga kura. Uchaguzi wetu unawafanya hata washindi washindwe kusherekea. Baada ya uchaguzi tunakumbana na internet black out.Tume ya ccm itampa ushindi Tundu lissu? Imerogwa?Nenda kokote, hapa hauko salama. Umejitahidi Kamanda kupambana. Nenda kapumzike usije ukafa kifo cha kipumbavu

  • Huku ni kutengeneza matukio tu ya kutafuta huruma na kuchafulia taifa heshima yake kwa masirahi yake binafsi. Baada ya kushindwa uchaguzi, kushindwa kuanzisha vurugu sasa anadai usalama wake upo hatarini….kwanini haukuwa hatarini wakati akitukana kwenye mikutano ya hadhara kwa siku 60 za kampeni. Huyu jamaa inawezekana si mzima.

  • Huyo lofa wa akili acha atapetape baada ya deal lake la kuuza nchi kushindwa. Alidhani watanzania ni mbumbumbu kama yeye aliyerubuniwa na wazungu kuwazuia nchi. Hakuna anayemtishia maisha yake, arudi tu kwa mabwana zake huyu shoga.

  • Mnadai hamna taarifa;kwani taarifa za kushambuliwa kwake 2017 hamkuzipata? Mmefanya nini mpaka sasa?? Mmemkamata nani? Tuwe honest jamani!

  • Tundu Lissu nenda mkuu ujihakikishie usalama wako. Mimi nafuatilia hotuba zako na press zako karibu zote. Siamini kama wewe ni muumini wa ushiga. Na umewahi kusema kwamba “mkate wako unaupata mahakamani na haujawahi kuona mtu amefungwa kwa ushoga”. Ulichosema ni haki ya kupata PRIVACY. Sasa hao wanaokusema wanafuatilia hayo? Hao wanaopinga ushoga wanawachukulia hatua gani hao mashoga? Mbona wapo tu kwenye jamii?!! Endelea na harakati zako, usiwasikilize wapuuzi. Usalama wako ni muhimu kaka.

  • Tundu Lissu nenda mkuu ujihakikishie usalama wako. Mimi nafuatilia hotuba zako na press zako karibu zote. Siamini kama wewe ni muumini wa ushiga. Na umewahi kusema kwamba “mkate wako unaupata mahakamani na haujawahi kuona mtu amefungwa kwa ushoga”. Ulichosema ni haki ya kupata PRIVACY. Sasa hao wanaokusema wanafuatilia hayo? Hao wanaopinga ushoga wanawachukulia hatua gani hao mashoga? Mbona wapo tu kwenye jamii?!! Endelea na harakati zako, usiwasikilize wapuuzi. Usalama wako ni muhimu kaka. Wanaocomment vibaya kuhusu Lissu kwa kiasi kikubwa hawajui wanachokizungumzia.

  • Tanzaniaeeeeeeeeeeeeeeeeee tongwe record baby
    Mimi nasoma comment nikimaliza naenda shamba.

  • Uchaguzi umeishaX3,watanzania tuelewe ,tujadili mbinu za maendeleo hasa sisi vijana muda ndo huu tukiwa bado na nguvu

  • Jueni kwamba ulimwengu huu tunaoishi unaongozwa na ulimwengu wa roho. Hivyo kila jambo ujue lilishapangwa, ulimwengu wetu unakamilisha tu, hatuwezi kubadilisha. Kuna unabii uliosema Atakuja na Atarudi . hayo ndio yanakamilika sasa.

  • Tatizo wapinzani tanzania hawana dhamira ya kweli juu ya nchi nchi yao,, ni wasaka tonge,,eti chama pamoja na ruzuku bado wamepanga..hawana mipango endelevu ya chama, bali wana mipango endelevu ya maisha yao na familiya zao, CCM itaendelea tu milele,,

  • Huyu jamaa Lissu ni Tapeli sana, amekula pesa za Wabelgiji kashindwa kuleta Vurugu Nchini, sasa Wabelgiji wanamtafuta arudishe Pesa zao anakimbilia Ubalozi wa Japani na Ujerumani! Kwanini asikimbilie Ubalozi wa Ubelgiji ambao ndiyo waliomtibu na Kumfadhili Uchaguzi? Namshauri arudishe Pesa za Wabelgiji ndiyo atapata Amani, Otherwise hata akimbilie wapi, Wabelgiji wanae tu!!😂

  • Nenda kwenye usalama rais lissu mung atatenda siku moja kwan weng tunamshtakia mung kwa haya yanayotokea tanzania maana imekua c tanzania yetu wananch ni ya baaz ya watu! Ila ony lang kwa waropokaj niwakumbushe tu hali inayokuja ni yetu sote tuivumilie tusije kuleta mdomo

  • Tanzania ni salama wale wenye nia ya tamaa ya madaraka wasumbili 2225 uchangunzi umekwisha sasa ni kuchapa kazi tu

  • Watanzania welevu wanajua nini maana ya uchaguzi, usalama, maendeleo nk. Ndiyo maana wakampata mshindi wao. Tuwapuuzie wanaolazimisha madaraka wakati hawana vigezo kwenye nchi yetu. Demokrasia ndiyo hiyo ya Watanzania, tusiige wala kufuata ya wengine kwani nao wana taratibu zao kwenye nchi zao. TUIPENDE, TUILINDE NA TUTUNZE SIRI ZA NCHI YETU TANZANIA.

  • Mataifa yanayotunza siri za nchi zao yako mbari kimaendeleo. kuropokaropoka ovyo ovyo ni kudhorotesha nchi yetu kwa kila kitu. TUIPENDE, TUILINDE NA TUTUNZE SIRI ZA NCHI YETU TANZANIA KWA MANUFAA YA WATANZANIA WOTE.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Rais Samia aridhishwa utendaji mabalozi, awapa neno

Spread the loveRais wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan amewapongeza mabalozi  wanaowakilisha ...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

NMB yadhamini Mkutano Mkuu ALAT, kufunguliwa na Samia

Spread the loveBENKI ya NMB, imekabidhi hundi yenye thamani ya Sh. 120...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mipango na uwekezaji kutumia bilioni 121.3, mradi wa Bagamoyo wapewa kipaumbele

Spread the loveWIZARA ya Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, imeliomba Bunge...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mbunge ataka kasi uzalishaji walimu ipunguzwe akidai hakuna ajira

Spread the loveMBUNGE wa Mlalo (CCM), Rashid Shangazi, ameishauri Serikali ipunguze kasi...

error: Content is protected !!