March 2, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Tume ya Uchaguzi Kenya yalegeza masharti

Wafula Chebukata, Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi na Mipaka ya Kenya (IEBC)

Spread the love

TUME ya Uchaguzi na Mipaka ya Kenya (IEBC), imeazimia kuongeza muda wa kupiga kura siku ya uchaguzi katika maeneo yenye sheria ya muda wa kutembea, anaandika Catherine Kayombo.

Akizungumza katika mkutano uliofanyika makao makuu ya tume jijini Nairobi, mwenyekiti wa tume, Wafula Chebukata amedokeza kuwa wasimamizi wa uchaguzi katika vituo husika wamekabidhiwa madaraka ya kuongeza muda wa kupiga kura katika vituo ambavyo kazi hiyo inaingiliwa na sababu nyingine halali.

“Kuchelewa kufunguliwa kwa vituo vya kupigia kura katika maeneo yanayoathiriwa na sheria ya kutembea kwa muda husika, kutafidiwa na utekelezaji wakanuni ya 64(1) na 63(1).

Maeneo yenye vizuizi vya muda ni pamoja na Garisa, Lamu na maeneo kando yam to wa Tana lile ambayo yanahusiwa kuwa si salama kuwepo kwa muda mrefu hasa katika kipindi cha uchaguzi.

error: Content is protected !!