Tuesday , 16 April 2024
Home Kitengo Michezo Tulia mgeni rasmi fainali Miss Tanzania
Michezo

Tulia mgeni rasmi fainali Miss Tanzania

Spread the love

NAIBU Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mbunge wa Mbeya Mjini, Tulia Akson atakuwa mgeni rasmi kwenye fainali ya Miss Tanzania itakayofanyika tarehe 5 Decemba, 2020 kwenye ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Mwalimu Nyerere, Dar es Salaam. Anaripoti Kelvin Mwaipungu, Dar es Salaam … (endelea).

Waaandaji na waratibu wa tamasha hilo kupitia taarifa yao wameeleza kuwa Naibu Spika huyo amethibitisha uwepo wake kwenye tukio hilo ambao umepewa kauli mbiu ya “Urembo ni heshima”

Shindano hilo ambalo linandaliwa na kampuni The Look litakuwa na warembo 20 watakaowania taji hilo kutoka sehemu mbalimbali nchini.

Waliofanikiwa kuingia katika fainali hiyo ni Prisca Lyimo (Ubungo), Tamia Hakamu (Arusha), Juliana Rugumisa (Arusha), Yvonne Paul (Kigamboni), Ruth Benitho (Ilala), Grace Machibula (Ubungo), Rose Manfere (Temeke), Margaret Mwambi (Kigamboni), Sarafina Mageye (Kinondoni).

Wengine ni Martha Golodi (Ubungo), Zenitha Chundu (Morogoro), Deolyn Mollel (Morogoro), Hoyce Bakanoba (Tabora), Necerian Kivuyo (Dodoma), Razia Abraham (Kinondoni), Angela Pendaeli (Arusha), Advera Mwemba (Mwanza), Verynice Deokari (Kinondoni) na Gloria Fela (Ilala)

Taji hilo kwa sasa linashikiliwa na Silvia Sebastian ambaye aliwakilisha kanda ya ziwa katika shindano hilo lililofanyika 2019, alifanikiwa kuondoka na Gari na kitita cha Shilingi 10 milioni kama zawadi.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Michezo

Anza Jumatatu yako na Meridianbet

Spread the love  IKIWA ni siku nyingine mpya kabisa ya Jumatatu baadhi...

Habari MchanganyikoMichezo

NBC, Yanga wazindua kadi  za kimataifa za uanachama

Spread the loveBenki ya Taifa ya Biashara (NBC) kwa kushirikiana na Klabu...

Michezo

TFF, Amrouche ngoma nzito

Spread the loveVIPENGELE vya mkataba wa kazi aliotia saini Kocha Mkuu wa...

Michezo

Jumapili ya maokoto na Meridianbet ni hii

Spread the love BAADA ya jana kushuhudia mitanange kibao kutoka ligi mbalimbali,...

error: Content is protected !!