Wednesday , 24 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Tujali, tuitunze miundombinu – Waziri Jafo
Habari Mchanganyiko

Tujali, tuitunze miundombinu – Waziri Jafo

Suleiman Jafo, Waziri wa Tamisemi
Spread the love

SERIKALI imetoa wito kwa Watanzania kutunza miundombinu nchini ili fedha zielekezwe kwenye maeneo mengine ya maendeleo. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma…(endelea).

Wito huo umetolewa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa( TAMISEMI), Selemani Jafo wakati akitoa mrejesho wa mafanikio yaliopatikana katika sekta ya miundombinu ndani ya miaka mitano (2015 – 2020) leo tarehe 5 Agosri 2020 jijini Dodoma katika wiki ya TAMISEMI.

Aidha Jafo amesema, ni wajibu wa kila Mtanzania kulinda miundombinu hiyo kwa kutoa ushirikiano kwa serikali pale ambapo kuna watu wanaokwenda kinyume na taratibu za utumiaji wa miundombinu iliopo katika maeneo yao.

“Wale wanaong’oa taa za barabarani, alama za barabarani,  wanaozidisha kipimo cha ubebaji mizigo kwenye barabara zilizojengwa mijini na vijijini, hao wote sio wema kwa nchi yetu kwani wanarudisha maendeleo ya Taifa letu nyuma,” ameeleza  Jafo.

“Neema hiyo ni kutokana na maono ya Rais John Magufuli aliyetoa kias cha shilingi Tirioni 3.6 kwa ajili ya kuboresha miundombinu mbalimbali ili wananchi wapate huduma za kijamii bila vikwazo,” amesema.

Katika hatu nyingine ameeleza, majukum makubwa na mafanikio ya sekta ya miundombinu chini ya TAMISEMI ni ujenzi wa machinjio ya kisasa, ofisi mpya za wakuu wa wilaya, nyumba za wakuu wa wilaya na ujenzi wa masoko ya kisasa  nchini.

Naibu Waziri TAMISEMI, Josephat Kandege amesema kuwa matunda ya mafanikio yote yanayoshuhudiwa na Watanzania ni kutokana na ushirikiano mzuri wa watendaji kwenye wizara hiyo.

“Mafaniko huletwa na ushirikiano mzuri baina ya watendaji, hivyo matokeo yake ni kupata malengo chanya kwa wananchi waliompa dhamana Rais Magufuli,” amesisitiza Kandege

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

THRDC yaongeza mkataba wa ushirikiano na ABA

Spread the love  MTANDAO wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC),...

Habari Mchanganyiko

Rufaa ya Equity Benki, State Oil yakwama

Spread the loveMAHAKAMA ya Rufani, jijini Dar es Salaam, imeshindwa kuendelea na...

Habari Mchanganyiko

Bodaboda waeleza mafanikio mafunzo usalama barabarani

Spread the loveMADEREVA bodaboda katika Jiji la Dodoma wameeleza jinsi mafunzo ya...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NBC yaahidi kuendelea kuunga mkono Serikali za Mitaa

Spread the loveBenki ya Taifa ya Biashara (NBC) imesisitiza dhamira yake ya...

error: Content is protected !!