Saturday , 20 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa TTCL yajitetea mbele ya JPM
Habari za Siasa

TTCL yajitetea mbele ya JPM

Rais John Magufuli
Spread the love

SHIRIKA la Mawasiliano Tanzania (TTCL) limekinzana na madai kwamba, linatoa gawio kwa serikalini licha ya kujiendesha kwa hasara. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Katika hafla ya kukabidhi gaiwo kwa mara ya pili kwa serikali leo tarehe 21 Mei 2019, Waziri Kindamba, Mkurugenzi Mkuu wa TTCL amesema, shirika hilo liko vizuri na kwamba, haliendeshwi kwa hasara kama inavyoelezwa na baadhi ya watu.

TTCL leo imemkabidhi Rais John Magufuli gawio la Sh. 2.1 Bilioni ikiwa ni ongekezo la Sh. 600 Milioni baada ya mwaka jana kukabidhi gawio la kiasi cha Sh 1.5 bilioni.

Kindamba amefafanua kuwa, kabla ya TTCL kutoa gawio serikalini, hesabu zake hukaguliwa na wakaguzi wa ndani waliobobea, kisha yanapitiwa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) ambaye anathibitisha kama mahesabu ni sahihi.

Amesema, baada ya hesabu hizo kuthibitishwa na CAG, Bodi ya TTCL hutoa ruhusa ya kiasi cha fedha za mapato ya shirika hilo kupelekwa serikalini kama gawio kwa mujibu wa sheria na muongozo wa Ofisi ya Msajili wa Hazina.

“Kuna mambo ambayo tunasoma katika magazeti na mitandao, maswali mengi yanaulizwa vipi ilikuwa hoi na kupotea kwenye ramani na leo iko katika ramani. Mahesabu haya hayajatengenezwa, sababu yamekaguliwa na kuthibitishwa na wahasibu wabobezi na baadaye yanakaguliwa na mkaguzi wa ndani,” amesema Kindamba na kuongeza;

“Kisha anapitia CAG ndiye anayethibitisha hesabu na kusema kitabu ni kisafi au kitabu kichafu, na ndivyo tunachokifanya baada ya wataalamu kupita. Tunakwenda kwenye bodi kuomba ridhaa ya kutoa gawio kwao, ni takwa la kisheria, na muongozo wa msajili wa hazing.”

Kuhusu hatua ya baadhi ya watu kuhusisha hasara iliyopata Kampuni Tanzu ya T-Pesa na TTCL, Kindamba amesema, hasara iliyopata kampuni hiyo haihusiani na mapato ya TTCL kwa kuwa, kila shirika linategemeana.

Hata hivyo, Kindamba amesema kampuni zinazohusika na biashara ya utoaji huduma za fedha mtandaoni hazipati faida pindi yanapoanza kazi.

“Hivi karibuni ilisemwa hasara ya kampuni tanzu ya T-Pesa, kibiashara makampuni ya ‘mobile money ‘ huwa hayapati faida kwa mara ya kwanza,  wanapfanya kazi mwaka wa pili wa tatu na baadae wanatengeneza faida,” amesema Kindamba na kuongeza;

“Kuna  watu wanachangaya, hizi ni kampuni mbili tofauti, sisi kama wanaTTCL tunapenda kukushukuru kwa kutupenda na malezi mazuri unayotupatia.”

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Rais Samia ataja mikakati ya kufikia trilioni 2 biashara Uturuki, Tz

Spread the loveWakati Tanzania na Uturuki zikidhamiria kuongeza kiwango cha biashara hadi...

BiasharaHabari za Siasa

Mavunde aagiza Perseus kuharakisha fidia Sengerema

Spread the loveWaziri wa Madini, Anthony Mavunde ameipongeza Kampuni ya Perseus kwa...

Habari za Siasa

Kigogo Chadema awanyooshea vidole vigogo serikalini kuhusu ripoti ya CAG

Spread the love  MWANACHAMA wa Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Boniface Jacob, amedai...

Habari za Siasa

Wabunge waikalia kooni TAKUKURU Bungeni

Spread the love  BAADHI ya wabunge wamelia na changamoto za utendaji wa...

error: Content is protected !!