Saturday , 20 April 2024
Home Kitengo Habari Kimataifa Trump yamemshinda, asalimu amri
Kimataifa

Trump yamemshinda, asalimu amri

Donald Trump, Rais wa Marekani
Spread the love

DONALD Trump, Rais wa Marekani ‘amezingirwa’ na sasa amesema, “nitakabidhi madaraka kwa amani.’ Inaripoti mitandaoya kimataifa…(endelea).

Kwa mara ya kwanza tangu kufanyika Uchaguzi Mkuu nchini humo, Trump amekiri kushindwa kwenye uchaguzi huo na sasa anajiandaa kuondoka.

Kiongozi huyo ‘mtata’ kwenye video yake aliyoiweka jana jioni Alhamisi ya tarehe 7 Januari 2021, amesema “niko tayari kukabidhi kwa amani.”

Katika video hiyo, hakutaja kabisa kuhusu madai yake ya awali ya kuibiwa kura ambayo yaliwachochea wafuasi wake kupiga kambi nje ya Ikulu ya Whitehouse na kuvamia Jengo la Capitol.

Wakati akitoa matamshi hayo, viongozi wa Chama cha Demokratik cha rais mteule wa taifa hilo, Joe Biden kinashinikiza Trump kung’olewa kwenye ofisi hiyo kabla ya muda kufika.

Soma zaidi hapa

Bunge la Marekani lavamiwa, risasi zarindima

Hoja zinazoporomshwa na vingozi hao ni kwamba, amekuwa akichochea wananchi kufanya uasi na vurugu hivyo kuligharimu Taifa hilo.

Baada ya saa 12 za kifungo cha ukurasa wake wa twitter, tayari mtandao huo umemfungulia ambapo ametumia ukurasa huo kulaumu wafuasi wake kwa uvamizi wa jengo hilo.

“Ni shambulio baya la waandamanaji waliovamia Bunge la Congress,” ameandika Trump.

Katika kanda hiyo mpya ya video alisema “sasa Bunge la Congress limeidhinisha matokeo na sasa utawala mpya utaingia tarehe 20 Januari.”

“Lengo langu sasa ni kuhakikisha kuwa mchakato wa kukabidhi madaraka unafanyika kwa njia ya amani. ‘Wakati huu tunahitaji maridhiano.”

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

KimataifaTangulizi

Mkuu wa majeshi Kenya afariki, Ruto atangaza maombolezo

Spread the loveRais wa Kenya, William Ruto ametangaza maombezo ya siku tatu...

Kimataifa

Majaji kuamua hatima ya Zuma leo

Spread the loveMajaji nchini Afrika Kusini leo Jumanne wataamua ikiwa rais wa...

Habari za SiasaKimataifa

Spika Afrika Kusini ajiuzulu kwa tuhuma za rushwa

Spread the loveSpika wa Bunge la Afrika Kusini, Nosiviwe Mapisa-Nqakula ametangaza kujiuzulu...

Habari MchanganyikoKimataifa

Tetemeko la ardhi laua 7, lajeruhi 800 Taiwan

Spread the loveWatu wapatao saba wamefariki dunia na wengine zaidi ya 800...

error: Content is protected !!