July 29, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Trump amejifunza kwa Bush?

Donald Trump, Rais wa Marekani

Spread the love

KAMA mji au jimbo litashindwa kuchukua hatua muhimu za kurejesha hali ya amani, basi nitatumia jeshi la Marekani kufanya kazi hiyo. Inaripoti Mitandao ya Kimataifa … (endelea).

Ni kauli ya Donald Trump, Rais wa Marekani inayojadiliwa kwa sasa hususan baada ya magavana kueleza, Rais huyo hana mamlaka hayo kisheria.

Ametoa kauli hiyo baada ya maandamano, vurugu na uporaji kushika kasi nchini humo, kutokana na polisi wa Minnesota kufanya mauaji ya Mmarekani mweusi George Floyd wiki iliyopita.

Swali linabaki, je Trump anaweza kuchukua hatua hiyo na iliwahi kuchukuliwa na rais yeyote kabla yake?

Robert Chesney, Profesa wa Sheria katika Chuo Kikuu cha Texas anasema, Trump anaweza kufanya hivyo na kwamba hatokuwa Rais wa kwanza kutumia jeshi ndani ya mipaka ya nchi hiyo.

Anafafanua, mwaka 1807 Marekani ilipitisha sheria kuruhusu Rais wa taifa hilo kutumia jeshi bila mamlaka za majimbo, na kwamba ila sharti ya kuwepo kwa hali ya hatari.

Akieleza chanzo cha kuundwa kwa sheria hiyo, Profesa Chesney amesema, mwaka huo yalitokea mashambulizi ya raia wa India.

“Sheria hiyo inasema, ridhaa ya magavana haitakiwi pale Rais anapothibitisha kuwa hali katika jimbo inawia ngumu kusimamia sheria nchini Marekani, au wakati haki za raia zinapotishiwa,” amesema.

Pia amesema, ipo sheria iliyopitishwa mwaka 1878 ikitaka mamlaka ya Bunge kuidhinisha matumizi ya jeshii, “lakini kuna sheria ya kupambana na vitendo vya uvamizi ina nguvu ya kusimama yenyewe, Rais huwa na mamlaka kisheria kupeleka jeshi bila kuomba idhini kutoka kwenye majimbo katika mazingira ya sasa.”

Kwa mujibu wa huduma ya utafiti ya bunge, sheria hii iliwahi kutumika mara kadhaa zamani, ingawa si kwa takribani miongo mitatu.

Tangu kupitishwa kwake, mara ya kwanza ilitumiwa na Rais mstaafu George HW Bush mwaka 1992 wakati wa vurugu za mji kwenye Los Angeles.

Mwaka 1957 Rais Dwight Eisenhower alitumia sheria hiyo lakini alikumbana na upinzani mkubwa kutoka kwa magavana.

Yeye alipeleka jeshi Arkansas kudhibiti maandamano ya wanafunzi.

error: Content is protected !!