Saturday , 20 April 2024
Home Habari Mchanganyiko TRA kuwashukia waendesha Bahati Nasibu
Habari Mchanganyiko

TRA kuwashukia waendesha Bahati Nasibu

Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipa Kodi, wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Richard Kayombo
Spread the love

MAMLAKA ya Mapato Tanzania (TRA), imeanza kutekeleza jukumu la kukusanya kodi kwenye michezo ya kubahatisha jukumu ambalo ilikabidhiwa kuanzia mwezi Julai mwaka huu anaandika Irene Emmanuel.

Akiongea na waandishi wa Habari leo jijini Dar es salaam, Richard Kayombo, Mkurugenzi Huduma na Elimu kwa Mlipakodi amesema kwamba kutokana na nmabadiliko hayo TRA itakusanya kodi katika michezo yote ya kubahatisha ikiwemo casino, sports betting, slot machines, lottery na kupitia ujumbe mfupi wa kwenye simu (sms).

“Mshindi katika bahati nasibu atakatwa asilimia 18 ya kiasi alichoshinda na kuwasilishwa TRA na mchezaji bahati nasibu huyo na kwa upande wa wachezeshaji kuwasilisha asilimia ya mapato, casino 15%, sports betting 6%, SMS na lottery 30%, National lottery 10% na vslot machines ni 32,000/- kila mwezi.” Kayombo Aliongeza.

TRA ikishirikiana na bodi ya michezo ya kubahatisha imetoa na inaendelea kutoa mafunzo kwa wananchi na waendeshaji wa michezo hiyo na piainatoa wito kwa wahusika wote kutoa ushirikiano ili kufasnikisha ukusanyaji wa mapato kwa ufanisi.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Gardner Habash wa Clouds Fm afariki dunia

Spread the loveALIYEKUWA mtangazaji wa kipindi cha Jahazi kinachorushwa na kituo cha...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Wauguzi, madaktari 1000 kugawiwa mitungi ya Oryx Gas

Spread the loveKAMPUNI ya Oryx Gas na Taasisi ya Doris Mollel Foundation...

Habari Mchanganyiko

Tanzania yachaguliwa Makamu wa Rais Tume ya Shirika la Hali ya Hewa Duniani

Spread the love  TANZANIA kupitia Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA)...

Habari Mchanganyiko

NEMC yaonya wanaojenga bila tathmini ya mazingira

Spread the loveBARAZA la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC),...

error: Content is protected !!