Friday , 29 March 2024
Home Habari Mchanganyiko TPA yatakiwa kupima mizigo kwa tani
Habari Mchanganyiko

TPA yatakiwa kupima mizigo kwa tani

Bandari ya Dar es Salaam
Spread the love

MBUNGE wa Baraza la Wawakilishi Jaku Hashim Ayoub (CCM) ameitaka Serikali kupitia Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) kuweka utaratibu wa kupima mizigo inayoingia bandarini kwa tani badala ya kupima kwa uzito wa shehena (CBM) ili kurahisisha upimwaji wa mizigo ya wafanyabiashara wa chakula kutoka Zanzibar, anaandika Dany Tibason.

Mbunge huyo alitoa kauli hiyo wakati akiuliza swali la nyongeza Bungeni ambapo pia alitaka kujua kama Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Edwin Ngonyani ili akaone changamoto zilizopo katika Bandari ya Dar es Salaam hali inayosababisha kampuni ya Haizap kushindwa kutekeleza majukumu yake.

“Naibu Waziri huoni kama wakati umefika sasa mizigo kupimwa kwa tani badala ya CBM ikizingatiwa Wazanzibar wanategemea sana chakula kutoka Bara na pia biashara kubwa iliyokuwepo Kati ya Zanzibar na Tanzania Bara na ndio Uchumi mkubwa wanaotegemea wazanzibar ukiacha zao la karafuu ambalo huzaa mwaka hadi mwaka?” alihoji Jaku.

Akijibu swali hilo, Mhandisi Ngonyani amesema vipimo vyote viwili vinatumika kutegemeana na aina ya mzigo ulivyopakiwa.

Kwa upande wake Mbunge wa Viti Maalum Mariam Msabaha (Chadema) alitaka kujua mikakati ya serikali ya kuondoa ukiritimba wa kutoza kodi mara kwa mara katika bandari ili wafanyabiashara wengi waweze kutumia bandari za hapa nchini kupitishia mizigo yao na kuiwezesha serikali kupata mapato.

Akijibu swali hilo, Mhandisi Ngonyani amesema upangaji wa bei huwa unashirikisha wadau wa bandari wakati wa upangaji wa bei na wakati wa kupitia upya bei hizo serikali itahakikisha inashirikisha wadau hao wa bandari.

Katika swali la msingi Jaku amesema vyakula kama mbatata, dagaa, mahindi, dawa za hospitali, vitunguu kuchajiwa kwa CBM ni kuwakandamiza kiuchumi wafanyabiashara.

Pia alitaka kujua kama nia ya serikali ni kuwakwamua wananchi kiuchumi au kuwakandamiza hasa ikizingatiwa kuwa baadhi yao ni wafanyabiashara wadogo.

Mhandisi Ngonyani amesema tozo zote bandarini huzingatia uzito (tonnege) au ujazo wa shehena (CBM) kwa mujibu wa kitabu cha tozo za Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari (TPA) ambapo viwango vya tozo vimelenga katika kuwasaidia wafanyabiashara kupata huduma bora.

Aidha amesema serikali siku zote imekuwa na nia ya kuwakwamua wananchi kiuchumi kwa kuweka mazingira mazuri kwa wananchi kufanya biashara zao kwa mujibu we sheria, kanuni na taratibu za utoaji huduma za bandari.

Mhandisi Ngonyani amesema serikali kupitia TPA imenunua vifaa vya ukaguzi wa mizigo, vifaa vya kuhudumia shehena na kuboresha maeneo ya kupumzikia abiria.

Vile vile amesema sababu za msingi kwa TPA kutoza tozo kisheria ni kurejesha gharama za utoaji wa huduma za bandari ili kufanya huduma hizo kuwa endelevu na kuendelea kuwekeza katika mifumo ya usimamizi ambayo itaongeza ufanisi.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Mtandao watetezi wa haki za mazingira Tanzania waundwa

Spread the loveMTANDAO wa watetezi wa haki za mazingira nchini Tanzania, umeundwa...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Kapinga kuongoza usambazaji wa mitungi ya gesi 10,000 ya Taifa Gas

Spread the loveNaibu Waziri wa Nishati, Judith Kapinga ameahidi kuongoza kwa ufanisi...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Wafanyabiashara, wawekezaji China waridhia kuwekeza bil. 800 katika sekta 5 nchini

Spread the loveUJUMBE wa wafanyabiashara na wawekezaji wakubwa kutoka Jimbo la Changzhou...

Habari Mchanganyiko

Bil. 4.42 kumaliza uhaba maji kata 2 Musoma Vijijini

Spread the loveWANANCHI wa kata za Busambara na Kiriba, Jimbo la Musoma...

error: Content is protected !!