Thursday , 25 April 2024
Home Habari Mchanganyiko TOSCI yadhibiti mbegu feki
Habari Mchanganyiko

TOSCI yadhibiti mbegu feki

Baadhi ya mifuko ya mbegu bora za kisasa
Spread the love

TAASISI ya kudhibiti ubora wa mbegu Tanzania (TOSCI) imefanikiwa kudhibiti uwepo wa mbegu feki baada ya kuimarisha matumizi ya lebo maalum ikiwemo kuweka nembo ya TOSCI na lebo ya uhakiki mipakani OECD tangu mwaka 2017 zoezi hilo lilipoanza. Anaripoti Christina Haule, Morogoro … (endelea).

Mtafiti Mwandamizi kutoka TOSCI, John Msemwa alisema hayo jana kwenye banda la TOSCI lililopo kwenye maonesho ya sikukuu ya wakulima 88 kanda ya Mashariki katika viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere ambapo alisema changamoto ya mbegu feki imepungua kwa kiasi kikubwa sasa.

Alisema pia changamoto hiyo imepungua kutokana na kuimarisha shughuli za ukaguzi katika maduka ya mbegu kote nchini.

Aidha Msemwa alisema zoezi hilo ni endelevu ambapo atakayekamatwa akiwa anauza mbegu feki atakuwa ameghushi na hivyo atachukuliwa hatua kwa mujibu wa sheria kanuni na taratibu zilizopo.

Msemwa alisema tatizo hilo la uuzwaji wa mbegu feki limekuwa likitokea zaidi kwenye maeneo ya mipakani au pembezoni mwa nchi ambayo ni mikoa ya Mbeya na Songwe na nyingine watu wanatengeneza wenyewe kienyeji na kuweka kwenye vifungashio jambo ambalo ni kosa kisheria.

Alisema Sheria ya mbegu inaruhusu mbegu kuzalishwa kutoka kwa Wakala wa Mbegu ASA au makampuni mengine kwa idhini ya ASA na kisha kuthibitishwa ubora wake na TOSCI na kama ni mbegu bora kupewa lebo ya utambulisho ya TOSCI na kwamba hiyo ni kwa mbegu zinazozalishwa ndani ya nchi.

Alisema kwa mbegu inayotoka nje ya nchi inapaswa kuwa na lebo maaluma ya kuthibitisha ubora wake kinyume na hapo hatua mbalimbali kwa mujibu wa kanuni na sheria zitachukuliwa dhidi ya muhusika.

Hivyo aliwataka wakulima kutumia mbegu bora kwa tija kwenye kilimo jambo litakalosaidia kukuza kipato chao na taifa kwa ujumla.

Hata hivyo aliwataka wadau na makampuni ya mbegu kufanya kazi zao kwa kufuata misingi, kanuni na taratibu za sheria ili kupata mbegu bora.

Hivyo aliwasisitiza wakulima kununua mbegu iliyokuwa na lebo ya TOSCI au lebo ya OECD (seed schemes) kwenye maduka au wakala aliye na cheti kwa kuuz ambegu kutoka TOSCI ili kuepuka kupata mbegu feki na hatimaye kupata hasara wakati wa mavuno.

Pia aliwataka wakulima kuhakikisha wanapewa risiti baada ya kununua mbegu ambayo wataitumia kama kielelezo pale tatizo litakapojitokeza.

Maonesho ya sikukuu ya wakulima 88 kanda ya mashariki yanafanyika katika  viwanja vya mwalimu Julius Nyerere vilivyopo eneo la Tungi , nje kidogo ya Manispaa ya Morogoro.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Exim Bank yatoa  vitanda kwa shule ya Jeshi la Polisi Moshi

Spread the love  BENKI ya Exim imekabidhii  seti ya vitanda kwa Shule...

Habari Mchanganyiko

NBC yakabidhi vitanda Shule ya Polisi Moshi

Spread the loveBenki ya NBC imekabidhi msaada wa vitanda 28 kwa Shule...

Habari Mchanganyiko

THRDC yaongeza mkataba wa ushirikiano na ABA

Spread the love  MTANDAO wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC),...

Habari Mchanganyiko

Rufaa ya Equity Benki, State Oil yakwama

Spread the loveMAHAKAMA ya Rufani, jijini Dar es Salaam, imeshindwa kuendelea na...

error: Content is protected !!