TMA yatabiri mvua hafifu mikoa 16 Tanzania

Spread the love

MAMLAKA ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), imetangaza mikoa 16 itakayopata mvua za vuli chini ya wastani hali itakayosababisha ukame katika maeneo hayo. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).

Utabiri huo, umetolewa leo Jumanne tarehe 8 Septemba 2020 na Mkurugenzi wa TMA, Dk. Agnes Kijazi wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.

Amesema, mvua hizo za vuli zinatarajia kuanza kunyesha kuanzia Oktoba hadi Desemba 2020.

Dk. Kijazi ameitaja mikoa hiyo 16 ni; Geita, Simiyu, Kagera, Mwanza, Shinyanga, Manyara, Arusha, Morogoro, Tanga, Dar es Salaam, Pwani, visiwa vya Unguja na Pemba, Kaskazini mwa Kigoma, Mara na Kilimanjaro.

Amesema, uchache wa mvua hizo unatokana na bahari ya Hindi kuna Lamina ambayo joto la bahari la wastani inatarajiwa maeneo ya upande wa magharibi mwa bahari ya Hindi wakati upande wa mashariki inatarajiwa kuwa na joto la bahari la juu ya wastani.

Dk. Kijazi amesema, mikoa ya Kaskazini mwa Kigoma, Simiyu, Geita, Mara, Mwanza, Kagera na Shinyanga inatarajiwa kukubwa na vipindi virefu vya ukame kutokana na kuanza wiki ya pili ya Septemba 2020.

Amesema, mikoa ya Pwani, Visiwa vya Unguja na Pemba, Dar es Salaam, Tanga, Kaskazini mwa Morogoro mvua zinatarajiwa kunyesha chini ya wastani hadi wastani kuanzia wiki ya nne ya Desemba 2020 ambapo kutakuwa na vipindi virefu vya ukame katika mikoa hiyo.

Bosi huyo wa TMA amesema, athari zinazoweza kujitokeza kutokana na upungufu wa mvua hizo ni upungufu wa unyevunyevu katika udongo, magonjwa ya milipuko, upungufu wa maji safi na salama, upungufu wa malisho na maji na kujitokeza migogoro ya wakulima na wafugaji.

Kuhusu kilimo na usalama wa chakula, Dk. Kijazi amesema, kutakuwa na upungufu wa unyevuunyevu katika udongo jambo ambalo litasababisha ukuaji hafifu wa mazao na uzalishaji kupunguza hivyo wakulima wanashauriwa kupanda mbegu na mazao yanayoweza kukomaa ndani ya muda mfupi.

Pia, amesema ukame huo unaotarajiwa kujitokeza utasababisha upungufu wa malisho na maji unaoweza kusababisha magonjwa ya milipuko kwa wanyamapori kutokana na ukosefu wa malisho na maji.

MAMLAKA ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), imetangaza mikoa 16 itakayopata mvua za vuli chini ya wastani hali itakayosababisha ukame katika maeneo hayo. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam ... (endelea). Utabiri huo, umetolewa leo Jumanne tarehe 8 Septemba 2020 na Mkurugenzi wa TMA, Dk. Agnes Kijazi wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam. Amesema, mvua hizo za vuli zinatarajia kuanza kunyesha kuanzia Oktoba hadi Desemba 2020. Dk. Kijazi ameitaja mikoa hiyo 16 ni; Geita, Simiyu, Kagera, Mwanza, Shinyanga, Manyara, Arusha, Morogoro, Tanga, Dar es Salaam, Pwani, visiwa vya Unguja na Pemba, Kaskazini mwa Kigoma, Mara na…

Review Overview

User Rating: 3 ( 1 votes)

About Regina Mkonde

2 comments

  1. 0625764596

  2. Acha tuuuuu. Ccm kunogileeeeee. Kiukweli magu ni rahisi anayetekeleza ahadi. Japooooo kuna changamoto kidogo kapitia mwanzoni. Wateule wake hawakumuelewa. Sasa awamu hiiiii kama mwenyekiti kachagua majembe kupigania ubunge. Tuwape kuraaa nyingi iliiiiiiiiii. Akafanye mengi zaidiiiiiiiiii.

Leave a Reply

Your email address will not be published.

error: Content is protected !!