Saturday , 20 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Tito Magoti ashtakiwa kwa uhujumu uchumi
Habari za SiasaTangulizi

Tito Magoti ashtakiwa kwa uhujumu uchumi

Spread the love

HATIMAYE mwanaharakati na Ofisa wa Elimu wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Tito Magoti, Theodory Faustine, wamefunguliwa mashitaka matatu likiwemo utakatishaji fedha kiasi cha Sh. 17 milioni. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Jeshi la Polisi limewafungulia kesi hiyo namba 137/2019 katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam leo tarehe 24 Desemba 2019, baada ya kuwashikilia kwa siku nne.

Makosa mengine yanayowakabili ni kushirikiana na magenge ya uhalifu pamoja na uhalifu wa mitandaoni.

Mpaka wanafikishwa mahakamani, Tito na mwenzake tangu wakamatwe, haikuelezwa walipelekwa katika kituo gani cha polisi. Juhudi mbalimbali zilifanywa na familia yake pia LHRC bila mafanikio.

Wakili Anna Henga, Mkurugenzi Mtendaji wa LHRC na familia ya Tito walitembelea vituo vyote vya polisi, lakini hawakufanikiwa kumwona ama kupata taarifa za wanaharakati hao.

Hata hivyo, tarehe 20 Desemba 2019, na SACP Lazaro Mambosasa, Kamanda wa Mkoa wa Dar es Salaam, aliuelezea umma kwamba, wanamshikilia mwanaharakati huyo.

Hakimu Mkazi Mkuu wa mahakama hiyo Janeth Mtega, ameahirisha kesi hiyo hadi tarehe 7 Januari, 2020 itakapotajwa.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari za Siasa

Mavunde aagiza Perseus kuharakisha fidia Sengerema

Spread the loveWaziri wa Madini, Anthony Mavunde ameipongeza Kampuni ya Perseus kwa...

Habari za Siasa

Kigogo Chadema awanyooshea vidole vigogo serikalini kuhusu ripoti ya CAG

Spread the love  MWANACHAMA wa Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Boniface Jacob, amedai...

Habari za Siasa

Wabunge waikalia kooni TAKUKURU Bungeni

Spread the love  BAADHI ya wabunge wamelia na changamoto za utendaji wa...

Habari za SiasaTangulizi

Mpina ataka Waziri Majaliwa ajiuzulu, akosoa teuzi za mawaziri

Spread the love  MBUNGE wa Kisesa, Luhaga Mpina, amemtaka Waziri Mkuu, Kassim...

error: Content is protected !!