Thursday , 28 March 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Tishio la uchumi kufuatia Corona: ACT yaziangukia jumuiya za kimataifa
Habari za Siasa

Tishio la uchumi kufuatia Corona: ACT yaziangukia jumuiya za kimataifa

Spread the love

CHAMA cha ACT-Wazalendo kimeziomba jumuiya za kimataifa, hususan taasisi za fedha, kuzipa nafuu katika ulipaji madeni, nchi masikini zenye mikopo, ili ziweze kupata fedha za kukabiliana na janga la mlipuko wa Virusi vya Corona. Anaripoti Faki Sosi, Zanzibar…(endelea).

Akizungumza na wanahabari visiwani Zanzibar, leo tarehe 4 Aprili 2020, Maalim Seif Sharif Hamad, mwenyekiti wa chama hicho, ameziomba taasisi hizo kusimamisha malipo ya mikopo, katika kipindi cha mwaka mmoja.

Maalim Seif amesema iwapo hilo litatekelezwa, nchi za Afrika zitatumia fedha hizo katika kujenga mfumo wa afya utakaosaidia watu masikini.

“Ninatumia nafasi hii basi kuomba jamii ya kimataifa na hasa Mashirika na Taasisi za Fedha duniani, kusaidia nchi zinazoendelea kwa kusimamisha kwa mwaka mmoja malipo ya madeni. Ili kutumia fedha zinazo okolewa kujenga mfumo wa afya utakaoweza kusaidia watu masikini,” amesema Maalim Seif.

Maalim Seif ameeleza zaidi kuwa, iwapo urejeshwaji wa mikopo utasitishwa katika kipindi hicho, Tanzania itabaki na Sh. 3 trilioni, ambazo zinaweza kusaidia wananchi na kulinda shughuli za biashara na uchumi.

“ Iwapo wakopeshaji watakubali kusimamisha malipo ya deni kwa mwaka mmoja tu, basi Tanzania itabakia na Shilingi Trilioni 3, ambazo zitatumika katika kuboresha huduma za afya kwa wananchi na kutoa msaada wa kulinda shughuli za biashara na uchumi,” amesema Maalim Seif..

Maalim Seif ameeleza zaidi kuwa “Tanzania ina deni la nje la jumla ya Dola za Marekani Bilioni 23 (sawa na shilingi Trilioni 53) ambapo asilimia 65% ya deni hili, inatoka kwa mashirika ya kimataifa na nchi wahisani. Kiasi kilichobakia ni mikopo kutoka kwenye mabenki ya biashara.

Ndiyo maana natoa wito kwa mashirika ya kimataifa kukubali kusimamisha Malipo ya deni lao, ili kuwezesha nchi zetu kukabiliana na mripuko huu, ambao unauwa watu na kuvuruga uchumi wa mataifa mbali mbali.”

Wakati huo huo, Maalim Seif amewataka Watanzania kuchukua tahadhari juu ya ugonjwa huo, hasa kufuata maelekezo ya namna ya kudhibiti ueneaji wake.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Nani anasema kuna hasara ATCL?

Spread the loveRIPOTI za makusanyo na matumizi ya fedha katika Kampuni ya...

Habari za SiasaTangulizi

CAG: Wastaafu, wenza wao chanzo NHIF kufilisika

Spread the loveRIPOTI ya ukaguzi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu...

Habari za SiasaTangulizi

Vikundi hewa 851 vyalamba bilioni 2.6 mikopo ya halmashauri

Spread the loveVIKUNDI hewa vya wajasirimali wadogo 851 kutoka katika halmashauri 19...

Habari za SiasaTangulizi

Mashirika matano yapata hasara mabilioni ya fedha

Spread the loveMASHIRIKA matano ya Serikali yanayojiendesha kibiashara, yamepata hasara ya mabilioni...

error: Content is protected !!