January 21, 2021

Uhuru hauna Mipaka

TFF yaeleza sababu Stars Vs Tunisia kucheza saa 4 usiku

Spread the love

KATIBU Mkuu wa Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania, (TFF) Wilfred Kidao amesema, haki za matangazo ya Televisheni ndio iliyosababisha mchezo kati ya Timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ dhidi ya Tunisia utachezwa saa 4:00 usiku. Anaripoti Kelvin Mwaipungu…(endelea).

Mchezo huo wa marudiano wa kundi J wa kuwania kufuzu michuano ya kombe la Mataifa huru ya Afrika (AFCON2021), utachezwa kesho Jumanne tarehe 17 Novemba 2020 Uwanja wa Benjamini Mkapa jijiji Dar es Salaam kuanzia saa 4:00 usiku.

Akizungumza mbele ya waandishi wa habari leo Jumatatu 16 Novemba, 2020 Kidao amesema, wao kama shirikisho walijitahidi kila namna kuomba Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) kurudisha nyuma muda wa mechi hiyo licha yakutoa sababu mbalimbali ikiwemo ya usalama lakini jambo halikufanikiwa.

“Ilipokuja jambo la kuweka mechi saa 4 usiku, CAF wao wakaja na hoja ya haki ya matangazo ya Televisheni na hawawezi kubadilisha na kama kuna changamoto za kiusalama wakasema tuingize asilimia 25 ya mashabiki” amesema Kidao.

Katibu Mkuu wa Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania, (TFF) Wilfred Kidao

Licha ya mchezo huo kupigwa muda huo lakini pia mashabiki watakao ruhusiwa kuingia ni nusu ya uwezo wa uwanja husika kama ilivyoanishwa kwenye kanuni za mashindano hayo yanayo milikiwa na CAF.

Stars inaingia kwenye mchezo huo huku ikiwa na kumbukumbu ya kupoteza kwa bao 1-0 kwenye mchezo wa ugenini dhidi ya Tunisia.

Ushindi kwa Stars kesho utakuwa na maana kubwa kwa kuwa utawaweka kwenye mazingira mazuri ya kufuzu kwenye michuano hiyo ambayo ni mikubwa kwa ngazi ya Timu za Taifa Barani Afrika.

Stars iko kundi J lenye timu nne ikiwa inashika mkia kwa pointi tatu sawa na Libya na Equatoria Guinea huku Tunisia ikiongoza ikiwa na polinti tisa

error: Content is protected !!