Wednesday , 24 April 2024
Home Habari Mchanganyiko TFDA waonya watengenezaji bidhaa feki
Habari Mchanganyiko

TFDA waonya watengenezaji bidhaa feki

Spread the love

MAMLAKA ya Uthibiti wa Chakula na Dawa (TFDA) imetoa angalizo kwa wauzaji, wasambazaji pamoja na watengenezaji wa bidhaa mbalimbali ambazo zipo chini ya usimamizi wa Mamlaka hiyo kutotengeneza bidhaa feki na badala yake watengeneze bidhaa ambazo haziwezi kusababisha madhara kwa watumiaji. Anaripoti Dany Tibason … (endelea).

Aidha wale ambao ni watumiaji wametakiwa kuwa walinzi waaminifu katika utoaji wa taarifa  katika mamlaka husika pale ambapo watabaini kuwa bidhaa zilizopo sokoni siyo sahihi na hazifai kwa matumizi.

Wito huo umetolewa na meneja wa TFDA, Kanda ya Kati, Dk. Mbekenga alisema kuwa afya ni mtu inatakiwa kulindwa na mtu mwenyewe kwa kuwa makini katika kile ambacho anakitumia kwa kuangalia muda na nenbo ya kile ambacho anakitumia kama muda wake haujaisha na kemikali zilizotumiaka ni sahihi.

Alisema kuwa kumekuwa na udanganyifu hasa kwenye vipodozi  kwa kutokuandikwa kwa  viwango vya kemikali vinavyotumika kutengenezea vipodozi jambo ambalo linapelekea watumiaji wengi kuathirika kwenye vipodo hivyo, mamlaka iliweza kubaini hilo hivyo inazidi kuwataadhalisha watumiaji wa vipodozi hususani wanawake.

Aidha alisema kuwa kwa asilimia kubwa TFDA imeweza kudhibiti bidhaa feki na zenye viambata vya sumu kutokana na kuwepo kwa hufatilia wa kina kwa ya bidhaa inayoingia sokoni kwa kuzalishwa ndani ya nchi au nje ya nchi.

Hata hivyo alisema kuwa bidaa ambazo zinabainika kuwa siyo sahihi ukusanywa na kupelekwa maabara kwa lengo la kupimwa viwango vyake na kutoa taadhari kwa mmiliki harari kwa lengo la kumtaadharisha kuwa makini na bidhaa ambayo anaizalisha kwa kkiwango ambacho kinakubalika, na ikiwa ni vile ambavyo vinzalishwa kutoka nje ukeketezwa.

 “Ili kuweza kubaini bidhaa ambazo hazifai mara nyingi huwa tunatuma wakaguzi kwenda kununua bidhaa kama wateja wa kawaida, alafu tunazirudisha maabara kuzikagua tena kama hazijachakachuliwa tunapobaini uchakachuaji hatua za kisheria hufuatwa,” alisema Dk. Mbekenga

Awali alisema kulikuwa na uvamizi na kunakiri hati miliki na kuchakachua bidhaa,na kuonekana stika ni sahihi lakini kilichopo ndani ya kasha husika ni kitu kingine ambacho wakati mwingine ubora wake ni haifai kabisa.

“Kutokana na hilo TFDA ilikuwa ikitoa ushauri kwa wamiliki halaliwa kutafuta wapelelezi wao ili kupambana  na uvamizi huo na baadae hatua za kisheria hufatwa japo ilikua ngumu katika upatikanaji wa wachakachuaji hao,” alieleza Dk. Mbekenga.

Dk. Mbekenga alibainisha kuwa madhara yanayowakumba watumiaji wa vipodozi vyenye viambata vya sumu ni pamoja na kuwasababishia, kansa ya ngozi, kansa ya maziwa, uharibifu wa figo na maini na pia kwa mama mjamzito husababisha  kuathiri mtoto katika mji wa mimba na kusababisha mtoto kuzaliwa akiwa mwenye ulemavu.

Aidha  alisema kuwa changamoto kubwa wanayokumbana nayo ni uingizwaji wa bidhaa kupitia mipakana  au kwa kutumia njia za panya kutokana na ukubwa wa nchi na alieleza kuwa wapo watu ambao wamekuwa wakisafirisha bidhaa feki kwa kutumia magari ya kusafirisha magari ya mafuta ambayo yanakuwa tupu.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Bodaboda waeleza mafanikio mafunzo usalama barabarani

Spread the loveMADEREVA bodaboda katika Jiji la Dodoma wameeleza jinsi mafunzo ya...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NBC yaahidi kuendelea kuunga mkono Serikali za Mitaa

Spread the loveBenki ya Taifa ya Biashara (NBC) imesisitiza dhamira yake ya...

Habari Mchanganyiko

Watuhumiwa 12 wa kilo 726.2 za dawa za kulevya wafikishwa mahakamani

Spread the love  WATUHUMIWA watatu wamefikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kibaha Mkoani...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mwekezaji amwaga bil. 39 kujenga viwanda 3 vya uchenjuaji

Spread the loveKampuni ya Mineral Access System Limited (MAST) inayoiwakilishwa kampuni ya...

error: Content is protected !!