Saturday , 20 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Tetesi za Ebola: WHO yatuma mjumbe Tanzania
Habari Mchanganyiko

Tetesi za Ebola: WHO yatuma mjumbe Tanzania

Spread the love

SHIRIKA la Afya Duniani (WHO), limetuma mjumbe wake Dk. Tigest Ketsela Mengestu nchini Tanzania, kwa ajili ya kufanya mazungumzo na serikali kuhusu tetesi za uwepo wa mlipuko wa ugonjwa wa Ebola. Anaripoti Martin Kamote…(endelea).

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo tarehe 24 Septemba 2019 na Dk. Hassan Abassi, Msemaji Mkuu wa Serikali, Tanzania ilimwita Dk. Mengestu ambaye anaiwakilisha WHO hapa nchini, ili kutoa maelezo kuhusu taarifa ya shirika hilo inayosambaa katika vyombo vya habari.

Hivi karibuni, ilisambaa taarifa ya WHO inayoeleza kwamba serikali ya Tanzania haitoi ushirikiano kwa shirika hilo, katika kufanya uchunguzi wa sampuli za watu wanaodaiwa kwamba wamefariki kwa ugonjwa wa Ebola.

Dk. Abbasi amekanusha madai hayo akisema kwamba, Dk. Mengestu amesema WHO haijasema na wala haina ushahidi wowote kuwa nchini Tanzania kuna Ebola.

“Serikali imemwita Mwakilishi wa Shirika la Afya Duniani (WHO) hapa nchini kupata kwa kina hoja za Shirika hilo zinazosambaa kupitia vyombo vya habari. Mwakilishi huyo amesisitiza kuwa WHO haijasema wala haina ushahidi wowote kuwa TZ kuna Ebola na itashirikiana na Serikali,” amesema Dk. Abassi.

Dk. Abbasi ameeleza kuwa, katika mazungumzo ya Dk. Mengestu na Dk. Damas Ndumbaro, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wamekubaliana kwamba WHO itafuata taratibu husika itakapotaka taarifa zaidi kuhusu suala hilo, kutoka serikalini.

“Aidha, katika mazungumzo hayo WHO imeafiki kuwa kama kuna mahitaji ya kupata taarifa zaidi kutoka Serikali ya Tanzania lazima utaratibu ulioanishwa katika miongozo ya taasisi hiyo na ambayo imeridhiwa na Serikali ifuatwe kikamilifu,” amesema Dk. Abassi.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari Mchanganyiko

Wauguzi, madaktari 1000 kugawiwa mitungi ya Oryx Gas

Spread the loveKAMPUNI ya Oryx Gas na Taasisi ya Doris Mollel Foundation...

Habari Mchanganyiko

Tanzania yachaguliwa Makamu wa Rais Tume ya Shirika la Hali ya Hewa Duniani

Spread the love  TANZANIA kupitia Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA)...

Habari Mchanganyiko

NEMC yaonya wanaojenga bila tathmini ya mazingira

Spread the loveBARAZA la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC),...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB Pesa Akaunti yawavutia wakaguzi wa ndani Afrika

Spread the loveUbunifu wa bidhaa bora wa Benki ya NMB pamoja na...

error: Content is protected !!