Friday , 19 April 2024
Home Habari Mchanganyiko TCRA yaifungia Clouds siku 7 
Habari MchanganyikoTangulizi

TCRA yaifungia Clouds siku 7 

Spread the love

MAMLAKA  ya Mwasiliano Tanzania (TCRA) imeagiza Clouds TV na Redio kusitisha matangazo yao kwa muda wa siku saba kuanzia kesho Ijumaa 28 Agosti hadi 3 Septemba 2020 kwa kosa la kukiuka kanuni za utangazaji na kanuni ndogo za utangazaji za uchaguzi. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).

Pia, mamlaka hiyo imevitaka Clouds TV na Redio kuomba radhi siku nzima ya leo Alhamisi tarehe 27 Agosti 2020 kwa kosa hilo.

Akizungumza na waandishi wa habari makamo makuu ya mamlaka hiyo, Mkurugenzi Mkuu wa TCRA, James Kilaba amesema, adhabu hiyo inatokana na kukiuka kanuni mbalimbali za utangazaji na kanuni ndogo za wakati wa uchahuzi za mwaka 2015.

Kilaba amesema, Clouds TV na Redio walikiuka kanuni za utangazaji kwa kutangaza wagombea kupita bila kupingwa wakati wenye uwezo wa kutangaza ni Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC).

“Mnamo tarehe 26 Agosti 2020 kati ya saa 1 hadi 4 asubuhi kupitia vipindi Clouds 360 na Powerbreakfast Clouds Redio. Walirusha takwimu za wagombea ubunge waliopita bila kupingwa lakini wakijua taarifa hiyo haijathibitishwa na NEC na kukosa pia midhania,” amesema Kilaba.

James Kilaba, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA)

Kutokana na ukiukwaji huo, Kilaba amesema, “kuanzia muda wa agizo hili saa 8 mchana leo mpaka mwisho wa siku hii ya leo, Clouds TV wanatakiwa kuahirisha matangazo yote na kutumia muda wote uliobaki kuomba radhi kwa Watanzania wote kwa kukiuka kanuni ya utangazaji kupitia kipindi chao cha Clouds 360.”

“TCRA imesitisha utoaji wa huduma za utangazaji kwa Clouds TV kuanzia kesho 28 Agosti 2020 hadi 3 Septemba 2020. Yaani hakuna kwenda hewani. Iwapo Clouds TV itashindwa au itakaa au itakaidi uamuzi huu, hatutakuwa na jinsi nyingine, tutachukua hatua zingine za kisheria na kiudhibiti,” amesema

Kilaba amesema, maagizo hayo kwa Clouds Tv yanafanyika pia kwa Clouds Redio kwa muda huo huo.

“Iwapo Clouds Redio itashindwa, itakaa au kukaidi, basi TCRA itachukua hatua za kisheria kati yao,” amesema Kilaba.

Mkurugenzi huyo amesema, “kwa kipindi chote cha uchaguzi, tuzingatie sheria na hii ni kwa vyombo vyote vya habari na pia zile za online.”

Pia, Kilaba ametumia fursa hiyo kutoa wito kwa watumiaji wa mitandao ya kijamii hususan makundi, “wananchama wa vyama vyote vya siasa kuzingatia matakwa ya kisheria kuhusu masuala ya uchaguzi tunapohusisha mitandao ya mawasiliano.”

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB Pesa Akaunti yawavutia wakaguzi wa ndani Afrika

Spread the loveUbunifu wa bidhaa bora wa Benki ya NMB pamoja na...

KimataifaTangulizi

Mkuu wa majeshi Kenya afariki, Ruto atangaza maombolezo

Spread the loveRais wa Kenya, William Ruto ametangaza maombezo ya siku tatu...

Habari Mchanganyiko

Carbon First, Ruangwa wasaini makubaliano ya biashara ya hewa ukaa

Spread the love  KAMPUNI ya Carbon First Tanzania Limited na Halmashauri ya...

Habari Mchanganyiko

CBE yawakumbuka wenye mahitaji maalum Jangwani

Spread the loveCHUO cha Elimu ya Biashara (CBE), kimetoa msaada mbalimbali na...

error: Content is protected !!