Friday , 26 April 2024
Home Habari Mchanganyiko TARI Hombolo waingia mkataba wa Mil 25 na TBL
Habari Mchanganyiko

TARI Hombolo waingia mkataba wa Mil 25 na TBL

Spread the love

KITUO cha Tafiti za mbegu bora za kilimo –TARI Hombolo, jijini Dodoma kimeingia mkataba wenye thamani ya dola za kimarekani 11,000 (zaidi ya Sh. 25 milioni) na kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kwa ajili ya kutafiti na kuzalisha mtama unaotakiwa katika kutengeneza bia. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma … (endelea).

Mkataba huo umeingia kati ya  ufadhili kutoka Shirika la Afrika ya Kusini la AB INBEV ambalo litakuwa likishirikiana katika shughuli zao za kila siku ndani ya mkataba huo.

Mtafiti na Mzalishaji Mkuu wa mbegu katika kituo cha tafiti za kilimo Tanzania (TARI), kituo cha Hombolo, Dk Lameck Nyaligwa alisema mkataba huo utasaidia kwa kiasi kikubwa sana kwa ajili ya kuzalisha mtama huo ambao unahitajia kwa ajili ya kuazalisha bia hapa nchini,.

Dk. Nyaligwa alisema wao kama TARI wamefurahi kupata mkataba huo huku akiwataka watanzania kukaa mnkao wa kula kutokana na kuwa watazalisha mbugu za mtama zilizobora ambazo zitakuwa na soko kwa ajili ya kutengeneza kinywaji aina bia.

“Tumefurahi kupata mkataba huo kwa sababu tunaamini utasaidia sana wakulima wa mtama kupta mbegu bora za mtama,” alisema Dk. Nyaligwa.

Alisema kilio cha wakulima ni kuhakikisha wanapata mbegu bora hivyo mkataba huo ni neema kwao kwa sababu wanauhakika wa kuzalisha mbegu ambazo zinahitajika katika kuzalisha mtama huo unaohitajika kutengeneza bia.

Hata hivyo alisema wakulima wanapaswa kuchangamkia fursa mara pale tu watakapoona mbegu hizo zimeanza kutole kwaajili ya watu kuanza kupanda mtama huo unaotakiwa kwa ajili ya bia.

Alifafanua zaidi ya kuwa hivi sasa wakulima wa mtama watakuwa na uhakika ya kuwa wakilima mtama huo watakuwa na mahali pa kuuzia kutokana na TBL kuwa pamoja nao katika zoezi hilo.

Mbali na kuwepo kwa utafiti wa kupata zao la mtama ambalo linafaa kwa utengenezaji wa kinywaji aina ya bia alisema kuwa mtama huo unaweza kufaa kwa chakula cha binadamu.

Alisema kuwa katika utafiti ambao unaendelea katika kituo cha TARI Hombolo ni pamoja na mtama ambao unafaa kwa malisho ya mifugo ambao unaweza kusaidia kumpatia ng’ombe maziwa ya kutosha pamoja na kumfanya kuwa na nyama nzuri.

Naye Mkulima wa zao hilo, Juma Lubeleje alisema wamekuwa wakihangaika na soko la mtama lakini hivi sasa wanaamini soko lao litakuwa kwa sababu mahali pa kuuza kupo.

Alisema wanaishukuru TBL kwa kuonyesha njia baada ya kuingia mkataba huo na shirika hilo pamoja na TARI ambapo wanaamini watakuwa wakombozi wa wakulima katika eneo hilo.

“Tumefurahi sana kupata neema hii tutajitahidi kulima kwa wingi ili tuweze kuuza mtama ambao utatusaidia katika kuongeza kipato na familia zetu,” alisema Lebeleje.

Alisema yeye na wakulima wenzie wanasubiri tu mbegu hizo zitoke ili waanze kuzitumia katika kupanda na baadae wakati wa mavuno watakuwa na uhakika wa soko la mtama ambao unahitajika kutengeneza kinywaji aina ya bia.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Wakili: Ukimpa zawadi mwenza marufuku kumpora hata mkiachana

Spread the love  WANANDOA na watu waliko kwenye mahusiano ya kimapenzi, wamekumbushwa...

Habari Mchanganyiko

Majaliwa: Mvua zimesababisha vifo vya watu 155, kuendelea hadi Mei

Spread the love  WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa amesema mvua kubwa za El-Nino...

Habari Mchanganyiko

Exim Bank yatoa  vitanda kwa shule ya Jeshi la Polisi Moshi

Spread the love  BENKI ya Exim imekabidhii  seti ya vitanda kwa Shule...

Habari Mchanganyiko

NBC yakabidhi vitanda Shule ya Polisi Moshi

Spread the loveBenki ya NBC imekabidhi msaada wa vitanda 28 kwa Shule...

error: Content is protected !!