Friday , 29 March 2024
Home Habari Mchanganyiko Tanzania yasaka maelezo Mtanzania ‘gaidi’ alivyojiua
Habari Mchanganyiko

Tanzania yasaka maelezo Mtanzania ‘gaidi’ alivyojiua

Kitanzi cha kunyonga
Spread the love

SERIKALI ya Tanzania imeiandikia barua Wizara ya Mambo ya Nje ya Kenya kutaka maelezo namna Rashid Charles Mberesero, alivyojiua katika gereza la Kamiti. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Talha Mohammed, Kaimu Balozi wa Tanzania nchini Kenya akizungumza na chombo kimoja cha habari jana tarehe 1 Desemba 2020 amesema, hawajapata majibu ya barua hiyo kutoka Wizara ya Mambo ya Nje ya Kenya.

“…tunaendelea kusubiri majibu kutoka Serikali ya Kenya kupitia Wizara ya Mambo ya Nje kuhusu mazingira ya kifo hicho,” amesema Balozi Mohammed.

Amesema, walielezwa kwamba Kenya inawasiliana na mamlaka zinazohusika kama Jeshi la Magereza ili kupata majibu sahihi ya tukio hilo.

Rashid na wenzake wawili wa nchini Kenya (Hassan Edin na Mohamed Abdi), walifikishwa mahakamani nchini humo na kuhukumiwa kifungo cha maisha baada ya kukutwa na hatia ya kuhusika kwenye shambulio la kigaidi katika Chuo Kikuu cha Garisa mwaka 2015.

Kwenye mkasa huo, magaidi hao wakishirikiana na kundi la kigaidi la Al – Shabaab, waliwapiga risasi wanafunzi zaidi ya 500 ambapo 150 kati yao, walifariki dunia.
Taarifa zaidi zinaeleza, baba wa marehemu Rashid, Mzee Charles Mberesero anafanya juhudi ili kupata mwili wa mwanaye.

Tayari amefika kwenye Ubalozi wa Kenya nchini Tanzania ili kupata maelezo namna anavyoweza kupata mwili wa mwanaye kwa ajili ya taratibu za maziko.

Ubalozi wa Kenya ulimweleza kwamba, afanye mawasiliano na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki kwa msaada zaidi, alikwenda wizara hiyo na kuanza taratibu za kupata mwili wa mwanaye.

“Mungu akipenda sisi kama familia, tutauchukua mwili wa mtoto wetu na kuuzika nyumbani,” amesema Mzee Mberesero.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

DAWASA waanza utekelezaji agizo la Samia

Spread the loveMamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam...

Habari MchanganyikoKimataifa

Zuma akataliwa kugombea urais

Spread the loveTUME Huru ya Uchaguzi Afrika Kusini (IEC) imemwondoa rais wa...

Habari Mchanganyiko

Mtandao watetezi wa haki za mazingira Tanzania waundwa

Spread the loveMTANDAO wa watetezi wa haki za mazingira nchini Tanzania, umeundwa...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Kapinga kuongoza usambazaji wa mitungi ya gesi 10,000 ya Taifa Gas

Spread the loveNaibu Waziri wa Nishati, Judith Kapinga ameahidi kuongoza kwa ufanisi...

error: Content is protected !!