Thursday , 25 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Tanzania yapata ‘dili’ uuzaji wa korosho
Habari Mchanganyiko

Tanzania yapata ‘dili’ uuzaji wa korosho

Spread the love

SHIRIKISHO la Korosho Barani Afrika (ACA), limeiteua Tanzania kuwa mwenyeji wa mkutano wa 13 wa wadau wa kimataifa wa korosho, unaotarajia kufanyika kuanzia tarehe 7 hadi 9 Novemba 2019. Anaripoti Regina Mkonde…(endelea).

Akizungumza na wanahabari leo tarehe 16 Julai 2019 jijini Dar es Salaam, Ernest Mintah amesema mkutano huo utatumika kama fursa kwa wakulima wa zao la Korosho Tanzania, ambapo wawekezaji kutoka mataifa mbalimbali wataweza kununua zao hilo.

Sambamba na hilo, Mintah amesema wadau wa korosho barani Afrika watautumia mkutano huo kutunga sera za kutatua changamoto za sekta ya korosho, ubunifu wa ubanguaji, utafiti wa uzalishaji pamoja na namna ya kuwezesha kiuchumi wakulima wa zao hilo.

Mintah amesema Tanzania itakua mnufaika mkuu wa mkutano huo, kutokana na kuwa nchi ya pili barani Afrika kwa kuzalisha korosho nyingi na zemye ubora wa kimataifa.

“Dhumuni la mkutano huo ni kuangalia hali ya upatikanaji wa fedha kwa wakulima na wadau wa korosho, kuboresha mifumo ya taarifa za korosho. Lengo ni kuhakikisha kwamba tasnia ya korosho Afrika inabakia kuwa mchangiaji anayeonekana ndani ya sekta,” amesema Mintah.

Dk. Steven Ngailo, Mkurugenzi wa Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania, akimuwakilisha Waziri wa Kilimo, Costantine Kanyasu, amesema serikali itahakikisha inatumia mkutano huo kama fursa ya kuitangaza nchi kimataifa.

“Tutahakikisha tunatumia fursa hiyo kutangaza nchi yetub kwamba Tanzania ni wazalishaji wa korosho. Tunategemea hawa wawekezaji wakija wawekeze. Wajenge viwanda vya ubanguaji korosho na kuongeza thamani zao la korosho,” amesema Dk.Ngailo.

Dk. Ngailo ameeleza kuwa, takribani kampuni 130 kutoka nchi 14 ambazo ni mwanachama wa ACA watashiriki katika mkutano huo.

Francis Alfred, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Korosho Tanzania amesema bodi hiyo imejipanga kuhakikisha kwamba korosho ghafi za msimu uliopita zilizohifadhiwa ghalani zinauzwa zote kabla ya msimu mpya kuanza, huku akibainisha kwamba watautumia mkutano huo kufanikisha zoezi hilo.

“Ile hazina tunaendelea kuuza ili mpaka unaisha huo msimu korosho, zote ziwe zishauzwa, kuna jitihada mbalimbali zinaendelea mpaka unaingia msimu mpya zisiwepo,” amesema Alfred.

Shirikisho la ACA lililoanzoshwa tangu mwaka 2005, kwa mara ya pili linafanya mkutano mkubwa na wa kimataifa Tanzania, ambapo mkutano wa kwanza ulifanyika mwaka 2008.

Dhumuni la mikutano wa mwaka huu ni kuchambua mabadiliko ya soko la korosho, mwitikio wa serikali na watendaji wa mnyororo wa thamani, kwa lengo la kuhakikisha kwamba kila mtu anawajibika kushughulikia changamoto zinazojitokeza kuhusu sekta ya Korosho.

Pia, washiriki watafanya ziara katika mikoa inayozalisha korosho, ikiwemo mikoa ya Kusini, Zanzibar na Dar es Salaam.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

THRDC yaongeza mkataba wa ushirikiano na ABA

Spread the love  MTANDAO wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC),...

Habari Mchanganyiko

Rufaa ya Equity Benki, State Oil yakwama

Spread the loveMAHAKAMA ya Rufani, jijini Dar es Salaam, imeshindwa kuendelea na...

Habari Mchanganyiko

Bodaboda waeleza mafanikio mafunzo usalama barabarani

Spread the loveMADEREVA bodaboda katika Jiji la Dodoma wameeleza jinsi mafunzo ya...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NBC yaahidi kuendelea kuunga mkono Serikali za Mitaa

Spread the loveBenki ya Taifa ya Biashara (NBC) imesisitiza dhamira yake ya...

error: Content is protected !!