Thursday , 28 March 2024
Home Kitengo Michezo Tanzania Prisons yakabidhiwa gari jipya
Michezo

Tanzania Prisons yakabidhiwa gari jipya

Basi jipya la timu ya Tanzania Prisons
Spread the love

KAMISHNA wa Magereza Tanzania, Jenerali Suleiman Mzee ameikabishi klabu ya Tanzania Prisons basi dogo aina ya Toyota Coaster itakayotumika na timu hiyo katika michezo mbalimbali ikiwamo Ligi Kuu Tanzania Bara. Anaripoti Kelvin Mwaipungu, Dar es Salaam … (endelea).

Katika makabidhiano hayo Mkuu wa sehemu ya michezo ndani ya jeshi hilo SSP Matrida Mlawa amesema kuwa wanamshukuru Jenerali Mzee kwa kuwapatia usafiri huo ambao utaisaidia timu na kutatua changamoto za usafiri.

“Tunamshukuru Jenerali wa Magereza, Kamanda Mzee kwa kuiwezesha kuipatia timu ya Tanzania Prisons gari ambalo litawasaidia katika safari kwenye michezo mbalimbali ikiwemo ya Ligi Kuu,” alisema Matrida.

 Aidha Matrida aliongezea kuwa wanaimani kubwa na Jenerali Mzee na wanamini ataisadia klabu hiyo ili iweze kusonga mbele.

Kwa sasa Prisons inashika nafasi ya nane, kwenye msimamo wa Ligi Kuu baada ya kujikusanyia alama 41 baada ya kucheza michezo 30.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Makala & UchambuziMichezo

TFF kuamua hatima ya Amrouche

Spread the loveHATIMA ya Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Adel Amrouche kuendelea...

Habari za SiasaMichezo

Matinyi: Dk. Ndumbaro alifanya utani ukaguzi mechi za Yanga, Simba

Spread the loveMsemaji Mkuu wa Serikali, Mobhare Matinyi amesema kauli iliyotolewa na...

Michezo

Gethsemane Group Kinondoni (GGK) waachia video ya Bwana Wastahili

Spread the loveWAIMBAJI maarufu nchini kutoka Gethsemane Group Kinondoni (GGK)SDA wameachia video...

BiasharaMichezo

Gamondi kocha bora mwezi Februari, NBC yamjaza manoti

Spread the loveBenki ya Taifa ya Biashara (NBC) ambae ni mdhamini Mkuu...

error: Content is protected !!