Thursday , 25 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Tanzania kuvuna asilimia 60 ya Bomba la Mafuta
Habari Mchanganyiko

Tanzania kuvuna asilimia 60 ya Bomba la Mafuta

Spread the love

SERIKALI ya Tanzania na ya Uganda zimekubaliana kuanza ujenzi wa Bomba la Mafuta Ghafi kutoka Hoima nchini Uganda hadi kwenye Bandari ya Tanga nchini Tanzania. Anaaripoti Faki Sosi …(endelea).

Makubaliano hayo yamefanyika leo tarehe 13 Septemba 2020 Chato mkoani Geita nchini Tanzania ambapo Rais Dk. John Magufuli wa Tanzania na Rais Yoweri Museveni wa Uganda wamekubaliana kuanza ujenzi huo huku Tanzania ikivuna faida ya asilimia 60 na Uganda ikinufaika kwa asilimia 40.

Rais Museveni amewasili nchini saa 6 mchana na kuondoka saa saa 7 na dakika 40 nchini baada ya kumaliza kutia saini makubaliano hayo.

Rais Magufuli amesema kuwa nchi hizo zimeafikiana kuchukua hatua kubwa kwenye maendeleo na uchumi wa nchi hizo.

Rais Dk. John Magufuli na Rais Uganda Yoweri Kaguta Museveni wakishuhudia mawaziri wa Nishati wa nchi zao (Mary Goretti
Kitutu-Uganda na Dkt.Medard Kalemani-Tanzania) wakitia saini
mkataba wa kuanza mradi wa Ujenzi wa Bomba la Mafuta kutoka
Hoima (Uganda)hadi Tanga leo

“Sehemu kubwa ya Bomba hili kilometa 1115 zipo upande Tanzania 330 zipo Uganda munaweza kuona umuhimu wa bomba hili kwa ustawi wa nchi zote mbili”

Amesema kuwa watu zaidi ya Elfu 90 watakaoguswa na mradi huo watalipwa fidia.

“Huu mradi ni historia nyingine ya pekee historia ya ushindi tulipomshinda Amani kwenye vita ya Tanzania na Uganda huu sasa ni ushindi wa Pili ushindi wa uchumi”, amesema Rais Magufuli.

https://www.youtube.com/watch?v=EsiIwUQb9iE

Amesema kuwa Tanzania itanufaika kwa asilimia 6 huku Uganda wakanufaika kwa asilimilia 40.

“Tumesaini tumekubaliana wataalamu wa Tanzania na Uganda wasituchelewesha , tunataka matokeo chanya …sasa nione wa upande wangu atakayetuchelewesha”, amesema Rais Magufuli.

Kwa muda mrefu bara la Afrika kuwa muhanga wa Taarifa hasi duniani , kuwepo kwa Vitaa , njaa, maradhi…mradi huu utaondoa dhana hiyo njaa na utavutia wawekezaji kuja kuwekeza kwenye nchi zetu hususan Afrika Mashariki.

Amesema kuwa Tanzania itatumia wataalam wa Uganda kufanya uchunguzi wa mafuta nchini.

Naye Rais Museveni amesema kuwa mradi huu utazinufaisha nchi hizo .

Amesema kuwa mbali na manufaa ya mafuta nchi hizo zitatafuta soko la pamoja kwa ajili ya nchi hizo.

Amesema kuwa nchi hiyo itarejea mezani kwa ajili ya mazungumzo ya gesi kutoka Tanzania kwenda Uganda.

Akizungumzia manufaa ya Bomba hilo Dk. Medard Kaleman Waziri wa Nishati amesema kuwa bomba hilo litakalo kuwa lenye urefu wa kilometa 1445.

Waziri Kaleman amesema kuwa bomba hilo litapita kwenye mikoa Wilaya 24 na vijiji 280  pia bomba hilo litakuwa na vipenyo venye nchi 24 na mapipa zaidi ya laki mbili.

Amesema kuwa  mbali manufaa mengine Tanzania itavuna kiasi cha Shilingi 7.8 Trilion kama mnafaika wa mradi huo.

Dk. Kaleman amesema mradi huo utawanufaisha Wanzania 10 elfu kwa kupata ajira.

Amesema  kuwa tayari  Serikali ishaafidia Shilingi 3 Bilioni ambapo wananchi 217 washafidiwa kutokana kuhamishwa kutoka unapopita mradi huo.

Akielezea makubaliano yaliyoafikiwa leo baina ya serikali hizo mbili Dk. Adelardus Kilangi Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Tanzania amesema kila nchi uchukue hatua za haraka za utiaji saini kwa kampuni zitakazohusika kwenye ujenzi wa bomba hilo.

“Kila nchi ichukue hatua ili kuwezesha utekelezaji wa ujenzi wa bomba la Mafua hayo ndio maelekezo ya msingi yaliyotolewa na Rais Museveni na Rais Dk Magufuli”

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Wakili: Ukimpa zawadi mwenza marufuku kumpora hata mkiachana

Spread the love  WANANDOA na watu waliko kwenye mahusiano ya kimapenzi, wamekumbushwa...

Habari Mchanganyiko

Majaliwa: Mvua zimesababisha vifo vya watu 155, kuendelea hadi Mei

Spread the love  WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa amesema mvua kubwa za El-Nino...

Habari Mchanganyiko

Exim Bank yatoa  vitanda kwa shule ya Jeshi la Polisi Moshi

Spread the love  BENKI ya Exim imekabidhii  seti ya vitanda kwa Shule...

Habari Mchanganyiko

NBC yakabidhi vitanda Shule ya Polisi Moshi

Spread the loveBenki ya NBC imekabidhi msaada wa vitanda 28 kwa Shule...

error: Content is protected !!