Tanesco yaidai serikali Sh. 125 bilioni

Share on FacebookShare on Google+Tweet about this on TwitterShare on LinkedIn

SHIRIKA la Umeme hapa nchini (TANESCO) limesema mbele ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), kuwa linaidai Serikali zaidi ya Sh. 125 bilioni 125 ambazo ni madeni baada ya ya taasisi mbalimbali kubwa za serikali kutumia umeme bila kulipa, anaandika Dany Tibason.

Tanesco imesema Shirika la Umeme Zanzibar (ZECO), ndiyo mdaiwa sugu kwani anadaiwa zaidi ya Sh. 85 bilioni huku taasisi nyingine za Serikali zikidaiwa Sh. 40 bilioni.

Felchesmi Mramba, mkurugenzi mtendaji wa Tanesco, amewaeleza wajumbe wa PAC kuwa shirika hilo linapata wakati mgumu kujiendesha kutokana na taasisi mbalimbali za serikali kutolipa kwa wakati madeni yanayotokana na matumizi ya umeme.

“Tumebaini kuwa Zeco inashindwa kutulipa kwa sababu inatoza gharama ndogo kwa watumiaji wa umeme Zanzibar tofauti na gharama za ununuaji umeme kutoka Tanesco na kwamba Zeco imewasilisha deni hilo kwa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) ili isaidiwe kulipwa,” amesema Mramba.

Msajili wa Hazina, Lawrence Mafuru, amesema tayari amewasilisha ripoti ya madeni hayo katika ngazi za juu za maamuzi ili yafanyiwe kazi.

“Tanesco imefanya jitihada kubwa kuhakikisha inalipwa madeni haya. Wiki mbili zilizopita tuliwasilisha suala hili kwa ngazi za juu za maamuzi na kueleza changamoto inayolikabili shirika hili kwa kutokulipwa madeni yake hasa na taasisi kubwa za serikali,” amesema Mafuru.

Naghenjwa Kaboyoka, mwenyekiti wa PAC, ameiagiza Serikali ihakikishe inalipa madeni yote ya Tanesco ndani ya kipindi cha miezi sita.

“Ni wakati Tanesco kujiendesha yenyewe kibiashara kwani kwa hali ya sasa ilivyo, haiwezekani mwananchi wa kawaida abanwe ili alipie bili ya umeme lakini taasisi kubwa za Serikali zilimbikize madeni,” amesema Kaboyoka.

Share on FacebookShare on Google+Tweet about this on TwitterShare on LinkedIn
SHIRIKA la Umeme hapa nchini (TANESCO) limesema mbele ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), kuwa linaidai Serikali zaidi ya Sh. 125 bilioni 125 ambazo ni madeni baada ya ya taasisi mbalimbali kubwa za serikali kutumia umeme bila kulipa, anaandika Dany Tibason. Tanesco imesema Shirika la Umeme Zanzibar (ZECO), ndiyo mdaiwa sugu kwani anadaiwa zaidi ya Sh. 85 bilioni huku taasisi nyingine za Serikali zikidaiwa Sh. 40 bilioni. Felchesmi Mramba, mkurugenzi mtendaji wa Tanesco, amewaeleza wajumbe wa PAC kuwa shirika hilo linapata wakati mgumu kujiendesha kutokana na taasisi mbalimbali za serikali kutolipa kwa wakati madeni yanayotokana…

Review Overview

User Rating: Be the first one !
0

About Dany Tibason

Visit Us On FacebookVisit Us On TwitterVisit Us On Youtube