Tanesco, REA wapigwa marufuku kuagiza vifaa nje – MwanaHALISI Online
Makao Mkuu wa Tanesco, Ubungo Dar es Salaam kabla hayajavunjwa
Makao Mkuu wa Tanesco, Ubungo Dar es Salaam kabla hayajavunjwa

Tanesco, REA wapigwa marufuku kuagiza vifaa nje

SHIRIKA la Umeme Tanzania (TANESCO) na Wakala wa Nishati Vijijini (REA) limetakiwa kusitisha uagizaji wa viunganishi vya miundombinu ya umeme (Accessories) kutoka nje ya nchi ifikapo mwezi Novemba mwaka huu. Anaripoti Regina Kelvin … (endelea)

Agizo hilo lilitolewa jana tarehe 6 Agosti, 2018 na Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani wakati alipotembelea Kiwanda cha uzalishaji viunganishi cha Auto Mech Ltd kilichopo Tabata jijini Dar es Salaam.

Dkt. Kalemani alitoa agizo hilo baada ya kujiridhisha kwamba kiwanda hicho kina uwezo wa kuzalisha viunganishi vya kutosha, ambapo aliitaka Tanesco kununua viunganishi vinavyotengenezwa hapa nchini.

 “Nimekuja hapa ili kujiridhisha kama Kiwanda hiki kina uwezo wa kuzalisha viunganishi vya kutosha, nimejiridhisha kuwa, kiwanda hiki kina uwezo wa kuzalisha viunganishi hivyo, kwa hiyo nimetoa miezi mitatu ili TANESCO, REA na Wakandarasi wote kwa pamoja wajiandae sasa kunua vifaa hivi nchini.” Alisema Waziri Kalemani.

SHIRIKA la Umeme Tanzania (TANESCO) na Wakala wa Nishati Vijijini (REA) limetakiwa kusitisha uagizaji wa viunganishi vya miundombinu ya umeme (Accessories) kutoka nje ya nchi ifikapo mwezi Novemba mwaka huu. Anaripoti Regina Kelvin ... (endelea) Agizo hilo lilitolewa jana tarehe 6 Agosti, 2018 na Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani wakati alipotembelea Kiwanda cha uzalishaji viunganishi cha Auto Mech Ltd kilichopo Tabata jijini Dar es Salaam. Dkt. Kalemani alitoa agizo hilo baada ya kujiridhisha kwamba kiwanda hicho kina uwezo wa kuzalisha viunganishi vya kutosha, ambapo aliitaka Tanesco kununua viunganishi vinavyotengenezwa hapa nchini.  “Nimekuja hapa ili kujiridhisha kama Kiwanda hiki kina…

Review Overview

User Rating: Be the first one !
0

About Regina Kelvin

Visit Us On FacebookVisit Us On TwitterVisit Us On Youtube