Friday , 19 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Takwimu ubakaji watoto zatisha
Habari Mchanganyiko

Takwimu ubakaji watoto zatisha

Naibu Waziri wa Kaitba na Sheria, Ummy Mwalimu
Spread the love

VITENDO vya ubakaji vimeongezeka kwa kasi kulinganisha na vitendo vingine vya ukatili wa kijinsia wanaofanyiwa watoto. Anaripoti Hamis Mguta…(endelea).

Kwa mujibu wa takwimu za Jeshi la Polisi mwaka 2018, matukio ya ubakaji ambayo yameripotiwa hadi mwaka huo ni 5,557. Matukio yanayohusu mimba yakiwa 2,692, ulawiti 1,159, shambulio 965 na kujeruhi 705 ambapo Tanga imeongoza ikifuatiwa na Mbeya, Mwanza, Arusha na Tabora.

Kauli hiyo imetolewa leo tarehe 31 Okotoba 2019 na Mwajuma Magwiza, Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Watoto kutoka Wizara ya Afya, kwenye kongamano kwa vyombo vya habari kuhusu ajenda ya kitaifa ya wajibu wa wazazi na walezi katika malezi na matunzo ya familia.

Amesema, kuongezeka kwa mmomonyoko wa maadili katika jamii na familia, ndio chanzo kikubwa cha matukio hayo kuongezeka.

Magwiza ambaye amemuwakilisha Ummy Mwalimu, Waziri wa Afya amesema, matukio ya ukatili kwa watoto yamekuwa yakiongezeka mara kwa mara huku wanaofanya ukatili huo, kwa kiasi kikubwa wakiwa watu waliokaribu na mtoto kama familia, ndugu, jamaa na rafiki.

“Kulingana na taarifa ya utafiti wa Afya ya Mama na Mtoto na viashiria vya Malaria ya mwaka 2015/16, inaonyesha kwamba asilimia 25 ya kaya za mijini na asilimia 27 ya kaka za vijijini, zina watoto ambao hawaishi na wazazi wao licha ya mzazi mmoja au wote wawili kuwa hai,’ amesema.

Hata hivyo, utafiti uliofanywa na Wizara ya Afya kwa kushirikiana na wadau wa watoto, kwa kipindi cha Desemba 2017 hadi Januari 2018, katika halmashauri 12 hapa nchini ilibaini uwepo wa watoto 6,393 wanaofanya kazi mitaani.

Na kwamba, kati ya hao, wasichana ni 1,528 na wavulana ni 4,865 ambapo utafiti huo ulibaini kuwa, watoto 1,385 wanaishi na kufanya kazi mitaani usiku.

“Kwa mujibu wa takwimu za Jeshi la Polisi za mwaka 2018, kuongezeka kwa vitendo vya ukatili kwa watoto kutoka 13,457 kwa 2017 hadi matukio 14,419 kwa 2018, ni sawa na ongezeko la asilimia 6.6. Vitendo hivyo vya ukatili ni pamoja na ulawiti, ubakaji, mimba, ndoa za utotoni, vipigo na ukeketaji vitendo,” amesema.

Hossen Kilonga, Baba wa watoto wawili katika familia ya watu watano, ameuambia mtandao huu kuwa utekelezaji wa Sheria ya mtoto (CRC), upo lakini hautiliwi mkazo.

Kilonga ameitaka serikali kushirikiana na taasisi mbalimbali zinazosimamia haki za watoto kutoa elimu kwa wazazi na walezi kusimamia malezi ya mtoto ili kuwalinda dcidi ya matatizo hayo.

“Ukikaa na kuzungumza na mtoto atakupa au atakuambia matatizo yake kama kuna matendo mabaya anafanyiwa wakati wewe haupo pengine na dada wa kazi au watu wengine wa karibu lakini wanaume wengi hawana tabia ya kufanya hivyo na hawala muda na watoto,” amesema Anna Msakuzi, mzazi wa mtoto mmoja.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB Pesa Akaunti yawavutia wakaguzi wa ndani Afrika

Spread the loveUbunifu wa bidhaa bora wa Benki ya NMB pamoja na...

Habari Mchanganyiko

Carbon First, Ruangwa wasaini makubaliano ya biashara ya hewa ukaa

Spread the love  KAMPUNI ya Carbon First Tanzania Limited na Halmashauri ya...

Habari Mchanganyiko

CBE yawakumbuka wenye mahitaji maalum Jangwani

Spread the loveCHUO cha Elimu ya Biashara (CBE), kimetoa msaada mbalimbali na...

Habari Mchanganyiko

Mume auwa mke kwa kumchoma visu, ajisalimisha Polisi

Spread the loveJACKSON Kalamji (49), anashikiliwa na Jeshi la Polisi jijini Mwanza,...

error: Content is protected !!