KATIKA hali isiyokuwa ya kawaida Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), imemugeuzia kibao Mbunge wa Arumeru Mashariki Joshua Nassari (Chadema) ambaye amewapelekea ushahidi wa namna Mkuu wa Wilaya ya Arumeru, Alexander Mnyeti alivyotumia rushwa kuwashawishi Madiwani wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kukihama chama hicho, anaandika mwandishi wetu.
Tofauti na ilivyotarajiwa na wengi kwamba taasisi hiyo ingeufanyia kazi ushahidi uliowasilishwa kwao na Mbunge huyo, lakini leo imemuonya mwanasiasa huyo na kumtaka asitoe aina yoyote ya shinikizo baada ya kuwapa ushahidi.
“Hii Taasisi haishinikizwi na mtu yeyote na hapaswi hata mara moja kutushinikiza…. natoa onyo jingine, endapo ataendelea na utaratibu huu tutachukua hatua za kisheria dhidi yake”
Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU, Valentino Mlowola, ametoa onyo hilo leo na kusisitiza kuwa hawafanyi kazi kwa shinikizo la mtu.
Nassari akiongozana na wabunge kadhaa wa Chadema wameiwasilisha ushahidi huo wa video kwa TAKUKURU ili iweze kufanya uchunguzi wake kwa mujibu wa sheria na taratibu.
Leave a comment