Takukuru kuwahoji wabunge 69 wa Chadema

Spread the love

TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) nchini Tanzania, inatarajia kuwahoji wabunge 69 wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kuhusu tuhuma za matumizi mabaya ya fedha, inazokikabili chama hicho. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam…(endelea).

Taarifa iliyotolewa leo Jumatano tarehe 10 Juni 2020 na Doreen Kapwani, Afisa Uhusiano wa Takukuru imesema mahojiano hayo yatafanyikia Makao Makuu ya taasisi hiyo Dodoma na yatakamilika wiki ijayo.

“Ni kweli kuwa Takukuru imewaita waheshimiwa wabaunge wa Chadema na waliowahi kuwa wabunge wa chama hicho kwa ajili ya mahojiano.”

“Hatua hii ni muendelezo wa uchunguzi wa malalamiko dhidi ya matumizi mabaya ya fedha nza Chadema unaoendeshwa na Takukuru ambapo hatua iliyopo sasa ni kuwahoji wabunge 69,” amesema Doreen

Taarifa hiyo ya Takukuru imekuja siku kadhaa tangu tuhuma hizo ziibuliwe na baadhi ya wabunge wa Chadema, hasa wale waliotangaza kukihama chama hicho.

Wabunge hao ni; Peter Lijualikali (Kilombero), David Silinde (Momba), Susan Masele na Joyce Sokombi (Wabunge Viti Maalumu), ni miongoni mwa wabunge walioibua tuhuma hizo, ambazo ziliungwa mkono bungeni na Spika Job Ndugai.

Doreen amesema, Takukuru inafanya uchunguzi huo kwa kuwa, inawezekana katika tuhuma hizo kukapatikana makosa ya ubadhirifu na ufujaji wa fedha za chama, na matumizi mabaya ya mamlamka.

“Fedha hizi zote ambazo zililalamikiwa na waliokuwa wabunge wa chama hicho ambao walitangaza kukihama, katika malalamiko yao, walidai walikuwa wakikatwa fedha katika mishahara yao kila mwezi kuanzia mwezi Juni 2016,” amesema Kapwani.

Doreen amesema, kwa mujibu ya malalamiko yao, wabunge wa viti maalum walikuwa wakikatwa Sh.1,560,00 na wabunge wa kuchaguliwa walikuwa wakikatwa Sh.520,000 na hawakuwa wanafahamu namna fedha hizo zilikuwa zikitumika.

Amesema kwa sasa Takukuru inamalizia kuwahoji viongozi wa Chadema, Bodi ya Wadhamini ya chama hicho, waliowahi kuwa viongozi, wabunge waliotoa taarifa na maofisa wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC).

TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) nchini Tanzania, inatarajia kuwahoji wabunge 69 wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kuhusu tuhuma za matumizi mabaya ya fedha, inazokikabili chama hicho. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam…(endelea). Taarifa iliyotolewa leo Jumatano tarehe 10 Juni 2020 na Doreen Kapwani, Afisa Uhusiano wa Takukuru imesema mahojiano hayo yatafanyikia Makao Makuu ya taasisi hiyo Dodoma na yatakamilika wiki ijayo. “Ni kweli kuwa Takukuru imewaita waheshimiwa wabaunge wa Chadema na waliowahi kuwa wabunge wa chama hicho kwa ajili ya mahojiano.” “Hatua hii ni muendelezo wa uchunguzi wa malalamiko dhidi ya matumizi mabaya ya fedha…

Review Overview

User Rating: Be the first one !

About Regina Mkonde

Leave a Reply

Your email address will not be published.

error: Content is protected !!