Friday , 19 April 2024
Home Kitengo Michezo Taifa Stars yatema watatu wa kimataifa
Michezo

Taifa Stars yatema watatu wa kimataifa

Kikosi cha Taifa Stars wakiwa mazoezini nchini Misri
Spread the love

TIMU ya taifa ya Tanzania (Taifa Stars), inayoshiriki michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika, inayotarajiwa kuanza tarehe 22 Juni mwaka huu, nchini Misri, imewaondoa katika kikosi chake wachezaji wake tisa, wakiwamo watatu wa kimataifa. Anaripoti Mwandishi Wetu, Misri … (endelea).

Taarifa zinasema, benchi la ufundi la Taifa Stars lilipokuwa likitoa orodha ya mwisho ya wachezaji 23 watakaoshiriki katika fainali hizo za AFCON, limemuacha kiungo mshambuliaji, Shiza Kichuya, beki Kiraka Abdi Banda na mshambuliaji Shaban Chilunda.

Pamoja na kwamba wachezaji hao watatu wanaocheza soka la kulipwa katika nchi za Hispania, Afrika Kusini na Misri, pamoja na kuteuliwa kwenye kikosi cha awali, lakini wameshindwa kupenya kwenye kikosi cha wachezaji 23 ambao kisheria ndio wanaopaswa kushiriki fainali hizo.

Baadhi ya mashabiki nchini hapa wanadai kuwa wachezaji muhimu waliofaa kushirikishwa katika mechi hizo wametemwa kwa sababu moja ama nyengine huku wengine wakikosa sababu zozote za kutoshirikishwa.

Kocha Mkuu wa Taifa Stars Emmenuel Amunike, amenukuliwa akisema, ameshindwa kumjumuisha Banda anayechezea klabu ya Baroka FC ya Afrika Kusini na badala yake ameamua kuwajumuisha kundini Ally Mtoni ‘Sonso’ wa Lipuli na nyota wa Mbao FC, Vincent Philipo.

Kwa upande mwengine, Kichuya anayechezea klabu ya ENPPI ya Misri, ameshindwa kufua dafu mbele ya Farid Mussa, Thomas Ulimwengu na Yahya Zayd.

Tenerife ya Hispania kwa kutopata nafasi ya kutosha ya kucheza, na badala yake kocha Amunike amemuita mshambuliaji aliyetimuliwa na klabu ya Botswana Defence Force XI, Rashid Mandawa.

Kwa upande mwengine benchi la ufundi la Taifa Stars lilimpatia nafasi mshambuliaji Adi Yussuf ambaye hivi karibuni alitia saini mkataba wa kujiunga na Blackpool inayoshiriki Ligi ya daraja la pili Uingereza.

Hata hivyo, hakukuwa na nafasi kwa nyota wa timu ya Taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 17 ‘Serengeti Boys’, Kelvin John kama ilivyo kwa kipa wa timu ya Taifa chini ya umri wa miaka 20, Claryo Boniface.

Nako nchini Afrika Kusini, beki wa nchi hiyo,  Brian Mandela, tayari alikuwa amewekwa nje baada ya kupata jeraha, ikimaanisha kwamba kocha Migne alikuwa na wachezaji wengine watatu zaidi wa kuwatema kutoka kikosi chake cha wachezaji 27 ambacho kilikuwa nchini Ufaransa kutoka tarehe 30 Mei.

Winga Christopher Mbamba atalazimika kusubiri ili kuiwakilisha Kenya kwa mara ya kwanza.

Mchezaji wa Ureno Winga Clifton Miheso alikuwa mwathiriwa mwengine katika kikosi cha mwisho cha Migne ijapokuwa ni kutemwa kwa Akumu ambako kumewashanagazaa mashabiki wengi.

Kiungo huyo wa kati amekuwa kiungo muhimu katika klabu yake ya Zambia ijapokuwa hajakuwa akishirikishwa mara kwa mara katika mechi nne za kufuzu katika kipute hicho tangu mkufunzi huyo wa Ufaransa alipochukua hatamu.

Mchezaji Allan Wanga ambaye amekuwa akiongoza katika ufungaji wa magoli katika ligi ya kenya pia ni miongoni mwa Waathiriwa wa shoka la kocha Migne .

Mbali na Wanga kipa wa kariobangi Sharks Brian Bwire ambaye licha ya kujumuishwa katika kikosi hicho hapo awali alizua mjadala mkubwa.

Hata hivyo, alitemwa katika kikosi hicho pamoja na kiungo wa kati wa AF leopard Whyvonne Isuza.

Mchezaji Musa Mohammed ambaye alipata jeraha katika mechi ya kufuzu kombe la Afcon dhidi ya Madagascar siku ya Ijumaa ameorodheshwa katika orodha hiyo pamoja na Abud Omar ambaye pia alipata jeraha dogo kabla ya mechi hiyo kukamilika.

Vile vile, hakukuwa na nafasi kwa mshambuliaji Shabani Chilunda ambaye hivi karibuni alivunja mkataba na klabu ya CD.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Michezo

Leo ni leo nani kutinga nusu fainali UEFA?

Spread the love HATIMAYE Jumanne ya UEFA imefika ambapo leo hii michezo...

Michezo

Anza Jumatatu yako na Meridianbet

Spread the love  IKIWA ni siku nyingine mpya kabisa ya Jumatatu baadhi...

Habari MchanganyikoMichezo

NBC, Yanga wazindua kadi  za kimataifa za uanachama

Spread the loveBenki ya Taifa ya Biashara (NBC) kwa kushirikiana na Klabu...

Michezo

TFF, Amrouche ngoma nzito

Spread the loveVIPENGELE vya mkataba wa kazi aliotia saini Kocha Mkuu wa...

error: Content is protected !!