
Wachezaji wa timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars
TANZANIA, Taifa Stars imeanza vibaya hatua ya mwisho ya mchujo kuwania kupangwa kwenye makundi ya kuwania tiketi ya kucheza Fainali za Mataifa ya Afrika 2015 zitakazofanyika nchini Morocco, baada ya kulazimishwa sare ya 2-2 na Msumbiji ‘Mambas’.
Katika mchezo huo, uliochezwa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam jioni ya leo, mabao ya Stars inayofundishwa na Mholanzi Mart Nooij yalifungwa na kiungo wa Azam FC, Khamis Mcha ‘Vialli’ aliyeingia kipindi cha pili kuchukua nafasi ya Mrisho Ngassa.
Kwa Matokeo hayo Stars itahitaji ushindi katika mchezo wake wa marudiano utakaochezwa mjini Maputo kati ya Agosti 1 na 3 mwana huu, au sare ya mabao 3-3 ili iweze kusonga kupangwa katika kundi F kujiunga na timu za Zambia, Carpe Verde na Niger.
Dakika 45 za kwanza zilimalizika bila bao na kipindi cha pili, Msumbiji walikuwa wa kwanza kupata bao dakika ya 47 kwa penalti iliyokwamishwa nyavuni na Elias Pelembe baada ya Kevin Yondan kucheza rafu kwenye eneo la hatari. Mcha aliisawazishia Stars bao hilo dakika ya 65 akimalizia kazi nzuri ya Thomas Ulimwengu.
Mcha tena akaifungia Stars bao lililoelekea kuwa la ushindi dakika ya 71 kwa penalti, baada ya mabeki wa Mambas kumchezea rafu Mbwana Samatta kwenye eneo la hatari.
Ntajifunza fantasy football….just for the angry Monday tweets
— POWER MABULAH (@IamNchaKALIH) July 20, 2014
Stars iliongeza mashambulizi langoni mwa Msumbiji na kukosa mabao kadhaa ya wazi. Msumbiji walizinduka na kufanya shambulizi zuri lililowapatia bao la kusawazisha dakika ya 87 kupitia kwa Isaac Carvalho aliyetokea benchi pia.
More Stories
Dk. Hoseah aomba kukutana na Rais Samia
Dk. Hoseah, wenzake waapishwa TLS
Zitto, Fatma Karume wazungumzia ushindi wa Dk. Hoseah TLS