Friday , 29 March 2024
Home Kitengo Maisha Afya Tahadhari ugonjwa wa surua yatolewa
Afya

Tahadhari ugonjwa wa surua yatolewa

Spread the love

WATANZANIA wametahadharishwa kuhusu mlipuko wa magonjwa ya kuambukiza kwa watoto ukiwemo ugonjwa wa surua, unaotajwa kuanza kuathiri nchi jirani. Anaripoti Regina Mkonde…(endelea).

Akizungumzia maadhimisho ya wiki ya chanjo jijini Dar es Salaam leo tarehe 25 Aprili 2019 katika semina maalum kwa waandishi wa habari juu ya uelewa wa chanjo, Mtaalamu wa Chanjo wa Shirika la Afya Duniani (WHO), Dk. William Mwengee amesema, kwa sasa ugonjwa wa surua umeanza kusambaa katika nchi za jirani.

Dk. Mwengee amesema, kasi ya kuenea kwa ugonjwa wa surua katika nchi zinazopakana na Tanzania imeongezeka kipindi cha kuanzia Januari hadi Machi 2019, ukilinganisha na kipindi kama hicho kwa mwaka jana.

“Asilimia 300 ya ugonjwa wa surua imeongezeka ukilinganisha na kipindi cha Januari hadi Machi 2018, wagonjwa wengi wametoka kwa jirani zetu ikiwemo Kongo-DRC, Sudan na Libya,” amesema.

Dk. Mwengee ameeleza sababu za kurudia kwa ugonjwa wa surua katika nchi za jirani, ikiwemo wananchi wa nchi husika kupuuzia chanjo dhidi ya magonjwa ya mlipuko.

Kufuatia hali hiyo, Dk. Mwengee ametoa wito kwa Watanzania kutopuuzia chanjo hasa kwa watoto wadogo ili kujikinga na maradhi ya kuambukiza.

“ Kinachosababisha magonjwa ya chanjo yajirudie, watu kupata mafanikio na kushindwa kuendeleza mafaniko. Watu wanaona hawaelewi hata ugonjwa ukoje, wanapoacha tunakua na watoto wengi ambao hawajachanjwa na kupelekea milipuko na vifo vingi na watoto kupofuka macho. Yote hayo yanasababishwa na kutokupata chanjo,” amesema Dk. Mwengee na kuongeza.

“Kwa Afrika imetuonesha kuna magonjwa ya kupooza kama polio na surua, haya magonjwa yanarudi, kifaduro yameanza kujitokeza kule ambako chanjo haziko vizuri, tuendelee kuthamini chanjo ambazo zina matokeo mazuri kule ambako watoto wamechanjwa.”

Meneja wa Mpango wa Taifa wa Chanjo wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Dafrossa Lyimo amesema serikali itahakikisha watoto wanapata chanjo ili kuwakinga na magonjwa hayo, kwa kuanzisha kampeni maalumu ya chanjo nchi nzima.

Amesihi wananchi kujitokeza kwa wingi kupeleka watoto wao kupata chanjo kampeni itakapoanza.

“Ni kweli tunaona kuna milipuko wa surua ya hapa na pale, sisi tunatakiwa kuandaa mkakati wa ziada wa kuhakikisha watoto wetu wanakinga. Mwaka huu tutafanya kampeni ya chanjo ya surua ili kuudhibiti tutakapotoa tarehe watu washiriki.

“ Wiki hii tunaadhimisha wiki ya chanjo duniani kote na hasa barani Afrika; tunaendelea kuhamasisha jamii kutumia huduma za chanjo kwa kuamini kuwa chanjo ni mkakati nafuu na wenye kutoa huduma bora kwa wananchi katika kupunguza vifo.”

Dk. Lyimo amesema wamekuwa wakitoa chanjo kwa magonjwa matano lakini kwa sasa idadi imeongezeka kufikia tisa za kuzuia magonjwa 13. “Tumefanikiwa kwa asilimia 99 katika utoaji wa chanjo duniani kote,” amesema Dk. Lyimo, huku akielezea ugumu wa baadhi ya watu katika kupeleka watoto wao kupata chanjo.

“Bado kuna watoto ambao tunaendelea kuhamasisha wafikishwe vituoni kupata chanjo kwa kuwa ni muhimu kukamilisha ratiba ya dozi tatu inayotakiwa… chanjo hizi zinatolewa bure kwa hivyo wazazi wajitokeze kupeleka watoto wao kupata chanjo,” amesema.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

AfyaHabari Mchanganyiko

Marekani kuipa Tanzania bilioni 980 kudhibiti VVU, UKIMWI

Spread the loveSERIKALI ya Tanzania inatarajiwa kupewa msaada wa fedha kiasi cha...

AfyaHabari Mchanganyiko

Wanavijiji wajenga zahanati kukwepa umbali mrefu kupata huduma

Spread the loveWANAVIJIJI wa Kata ya  Musanja Jimbo la Musoma Vijijini, mkoani...

AfyaTangulizi

Wanasayansi wagundua teknolojia ya kunyofoa VVU kutoka kwenye seli

Spread the loveTIMU ya wanasayansi kutoka Chuo Kikuu cha Amsterdam cha nchini...

Afya

Wananchi 530,000 kufaidika na ujenzi wa hospitali ya bil. 1.8

Spread the love  SERIKALI imetoa Sh 1.8 bilioni kwa ajili ya ujenzi...

error: Content is protected !!