Joseph Mbilinyi 'Sugu' akiwa mahakamani akisikiliza hukumu yake

Sugu, Masonga wahukumiwa miezi mitano jela

MBUNGE wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi (SUGU) na Emmanuel Masonga, Katibu wa Kanda ya Nyasa Chadema, wamehukumiwa kwenda jela miezi mitano kwa kosa la uchochezi. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Hukumu hiyo imetolewa na Hakimu Mkazi wa Mahakama hiyo, Michael Mteite, baada ya kujiridhisha kuwa watuhumiwa hao wana hatia dhidi ya kesi ya kutumia lugha ya fedheha kwa Rais John Magufuli

Sugu pamoja na Masonga walifikishwa mahakamani hapo kwa mara kwanza Januari 19, 2018, kwa kosa hilo walitoa kauli hizo katika mkutano wa hadhara walioufanya Desemba 30 mwaka jana wakiwa viwanja vya Shule ya Msingi Mwenge jijini Mbeya.

Maneno yaliyomtia hatiani Sugu na mwenzake ni “Mhe Rais Magufuli hawezi kupendwa na watu kwa kumshoot risasi Lissu, kumtupa Jela miezi minne Lema, kumteka Ben saanane, kumteka Roma na kumzuia SUGU asiongee.”

MBUNGE wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi (SUGU) na Emmanuel Masonga, Katibu wa Kanda ya Nyasa Chadema, wamehukumiwa kwenda jela miezi mitano kwa kosa la uchochezi. Anaripoti Mwandishi Wetu ... (endelea). Hukumu hiyo imetolewa na Hakimu Mkazi wa Mahakama hiyo, Michael Mteite, baada ya kujiridhisha kuwa watuhumiwa hao wana hatia dhidi ya kesi ya kutumia lugha ya fedheha kwa Rais John Magufuli Sugu pamoja na Masonga walifikishwa mahakamani hapo kwa mara kwanza Januari 19, 2018, kwa kosa hilo walitoa kauli hizo katika mkutano wa hadhara walioufanya Desemba 30 mwaka jana wakiwa viwanja vya Shule ya Msingi Mwenge jijini Mbeya. Maneno yaliyomtia hatiani…

Review Overview

User Rating: Be the first one !

About Mwandishi Wetu

Visit Us On FacebookVisit Us On TwitterVisit Us On Youtube