January 21, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Stars, Tunisia mashabiki ruksa

Spread the love

SHIRIKISHO la mpira wa miguu barani Afrika (CAF) limeruhusu mashabiki kuingia uwanjani kwenye mchezo kati ya timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) dhidi ya Tunisia utakaopigwa kwenye Uwanja wa Benjamini Mkapa, jijini Dar es Salaam. Anaripoti Kelvin Mwaipungu… (endelea)

Mchezo huo ambao utakuwa wa kusaka tiketi ya kufuzu kwenye kombe la mataifa huru ya Afrika utachezwa 17 novemba 2020.

Taarifa kutoka ndani ya Shirikisho la Mpira wa miguu Tanzania (Tff) imeeleza kuwa CAF imetoa maelekezo kuwa idadi ya watazamaji watakaruhusiwa kuingia katika mchezo huo ni asilimia 50 ya uwezo wa Uwanja husika.

TFF baada ya taarifa hiyo imeeleza kuwa itawasiliana na serikali ambao ni wamiliki wa uwanja huo ili kutimiza matakwa ya CAF katika mchezo huo wa marudiano.

Ikumbukwe hapo awali CAF ilipiga iliweka katazo la mashabiki kuingia viwanjani katika michezo yote ya kusaka tiketi ya Afcon inatotarajiwa kuchezwa hivi karibuni huku ukiwa muendelezo wa kupambana na ugonjwa wa Covid-19.

Katika kuelekea kutafuta tiketi hiyo tayari kikosi cha Taifa Stars tayari kinaendelea na kambi ya siku tatu nchini Uturuki ambapo wanajiandaa na mchezo wa duru la kwanza dhidi ya Tunisia utakaochezwa 13 Novemba 2020 kwenye mji wa Tunis.

error: Content is protected !!