July 26, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Spika Ndugai, Mwambe wapeta

Spika wa Bunge, Job Ndugai

Spread the love

MAHAKAMA Kuu Masjala ya Dar es Salaam imetupilia mbali kesi ya kikatiba ya kupinga uamuzi wa Job Ndugai, Spika wa Bunge kumrejesha bungeni aliyekuwa mbunge wa Ndanda, Cecil Mwambe. Anaripoti Faki Sosi, Dar es Salaam … (endelea). 

Katika kesi hiyo ya kikatiba namba 10 ya mwaka 2020, ilifunguliwa na wakili wa kujitegemea Paul Kaunda, dhidi ya Spika Ndugai, Mwambe na Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), kupinga uamuzi Mwambe kurejeshwa bungeni wakati si mbunge halali.

Wakili Kaunda aliiomba mahakama hiyo itengue kauli ya Spika Ndugai kumtambua Mwambe mbunge halali, kwa kuwa alitangaza kujivua uanachama wa Chadema.

Amesema, Mwambe alijiunga CCM na kwamba baada ya kujivua uanachama, alijivua ubunge kwa mujibu wa ibara ya 71(1)(f) ya Katiba.

Awali, serikali iweka pingamizi ikiiomba mahakama isiisikilize kesi hiyo, ikibainisha hoja tano, pamoja na mambo mengine ikidai kuwa mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza kesi hiyo na kwamba kesi hiy ina kasoro za kisheria.

Leo tarehe 3 Juni 2020, Jaji Issa Maige akishirikiana na Jaji Stephen Magoiga na Jaji Seif Kulita amesema, mlalamikaji alikosea namna ya kufungua kesi ya kikatiba badala yake alipaswa kufungua kesi kwa utaratibu wa kawaida.

Jaji amesema, kauli ya Spika Ndugai aliyoitoa haikuwa imevunja Katiba bali ni ya kiutaratibu katika shughuli zake za kiutendaji, hivyo mlalamikaji angekuwa sahihi kama angefungua kesi hiyo kwa utaratibu wa kawaida kwa kutumia Ibara ya 83 (1) badala ya ile ya 26 (2) aliyoitumia.

Katika Ibara ya 83 (1) inaeleza kila shauri kwa ajili ya kupata uamuzi juu ya suala (a) kama uchaguzi au uteuzi wa mtu yeyote kuwa mbunge  ulikuwa halali au sivyo; au (b) kama Mbunge amekoma kuwa mbunge na kiti chake katika Bunge ki wazi au hapana, litafunguliwa na kusikilizwa kwanza katika Mahakama Kuu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania bila ya kuathiri masharti ya  ibara ndogo ya (2).

(2) Iwapo Tume ya Uchaguzi katika kutekeleza madaraka yake kwa mujibu wa masharti ya ibra ya 41(3) ya Katiba hii imemtangaza Mbunge yeyote kwamba amechaguliwa kuwa Rais basi hakuna mahakama wala chombo chochote kingine kitakachochunguza zaidi suala lolote linalohusu kiti cha Mbunge huyo kuwa wazi.

Jaji Maige amesema, ibara hiyo inaenda sambamba na kifungu cha 37 cha Sheria ya Uchaguzi, ambacho kinaeleza kuhusu utaratibu wa kutangaza kiti cha mbunge ambacho kiko wazi.

Wakati huo huo, mahakama ikisikiliza shauri namba 12 la mwaka 2020, lililofunguliwa na Shirika la Uraia na Msaada wa Sheriaa (Cilao) na kulipangia tarehe 11 Juni kwa ajili ya kuendelea na usikilizwaji.

Shauri hilo linafanana na lile la Kaunda, kwamba Cilao imemshtaki Spika Ndugai kuwa kauli yake ya kumtambua Mwambe kama mbunge inavunja Katiba.

Mbali na Spika Ndugai shirika hilo limemshtaki Mwambe na Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

Mahakama hiyo imewapa muda mawakili wa Shirika hilo kupitia uamuzi wa shauri la Kaunda ili ikifika tarehe 11 Juni waweke msimamo wa kuendelea ama la kwa kuwa mashauri hayo yanafanana.

error: Content is protected !!